![]() |
Advertisement |
Lusaka, Zambia. Mabingwa wa Zambia, Zesco United watamthibisha George ‘Chicken’ Lwandamina kuwa kocha wao wakati wowote leo Jumanne.
Kwa mujibu wa mtandao wa http://zambianfootball.co.zm/
kocha huyo wa zamani wa Chipolopolo Boys tayari amesaini mkataba wa awali kwa ajili ya kuchukua jukumu hilo mwezi ujao.
Lwandamina mkataba wake na Yanga utamalizika mwisho wa mwezi Mei.
“Labda Lwandamina na Yanga wafikie makubaliano, basi atajiungo na Zesco mwezi ujao,” chanzo hicho kiliiambia ZamFoot Crew leo Jumanne.
Tayari kocha wa sasa wa Zesco United, Tenant Chembo amejiuzuru, lakini Katibu mkuu mpya wa klabu hiyo Richard Mulenga amesema hana taarifa za kujiuzuru huko.
“Jambo hili limetokea mapema sana kuhusu kujiuzuru kwa TC (Tenant Chembo).
“Tulitegemea tungekuwa naye TC hapa hadi mwisho wa Mei kabla ya Lwandamina kuchukua jukumu hilo.”
Baada ya Chembo kuondoka msaidizi wake Emmanuel Siwale anategemea Zesco kesho Jumatano dhidi ya Lusaka Dynamos kwenye Uwanja wa Sunset.
Hata hivyo kocha huyo wa mambingwa mfululizo wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans amekanusha taarifa hizo
Lwandamina ameliambia Mwanaspoti jana kuwa, bado yuko Yanga na hajutii kuwepo kwake kwa kuwa uamuzi wake. Kibarua cha kocha wa Zesco kipo wazi baada ya aliyekuwepo kubwaga manyanga juzi baada ya matokeo mabovu ya timu yake.
Hata hivyo, Lwandamina amsema kule Zambia karibu nusu ya klabu zinataka huduma yake kutokana na rekodi zake bora, lakini hajafikiria kuiacha Yanga na akili yake ni kushinda mataji na kutamba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
“Nimesikia hizo taarifa (Anacheka) hakuna ukweli kuwa naondoka hapa kama ingekuwa hivyo ningefanya muda mrefu sana ila nimeamua kubaki Yanga kwa maamuzi yangu.
“Zambia kila wakati napokea ofa za timu kuhitaji nikafanye kazi na nina ofa nyingi sana, lakini ukweli bado nipo Yanga natumikia mkataba wangu,î alisema.
0 maoni: