![]() |
Advertisement |
Wamiliki wa Swansea wamemuuliza Carlos Carvalhal iwapo yuko tayari kuwaongoza. (Independen
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema anamtakia mema kocha Mikel Arteta huku kukiendelra na uvumi kuwa Arteta 36, anatarajiwa kuchukua mahala pake Arsene Wenger.
Kipa wa Slovakia Martin Dubravka, 29, atafanya mazungumzo na Newcastle United siku zinazokuja baada ya kumaliza mkopo wake kutoka Sparta Prague.(Chronicle Live
Meneja wa Leicester Claude Puel amesema kuwa ataheshimu mkataba wake na klabu hiyo licha ya uvumi kuwa anatafutwa na klabu ya Ufaransa Saint-Etienne. (Leicester Mercury)
Meneja wa Everton Sam Allardyce amesema hakuna mzozo kati yake na Wayne Rooney, wakati mchezaji huyo wa miaka 32 anahusihswa na klabu ya ligi kuu ya soka ya DC United. (Talksport)
David Wagner amekataa kutoa hakikisho lolote kuhusu hatma yake kama meneja wa Huddersfield licha ya mwenyekiti wake Dean Hoyle kusema atasalia katika klabu hiyo. (Mirror)
Mashabiki wa AC Milan walikataa kuchukua shati lake kipa wa miaka 19 raia wa Italia Gianluigi Donnarumma wakati wa kumalizika kwa mechi ya siku ya Jumamosi na Atalanta.
Mchezaji wa zamani wa Stoke Dominic Matteo anaamini klabu hiyo ingemfuta meneja Mark Hughes mapema ili kuzuia klabu hiyo kuzushwa kutoka kwa Premier League. (Inside Futboll
Manchester United wana mpango wa kumchukua mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar huku klabu hiyo ya Old Trafford ikipambana na Real Madrid kupata sahihi ya mchezaji huyo 26 mwenye asili ya Brazil (Sunday Mirror)
Unai Emery, ambaye ataondoka Paris St-Germain mwishoni mwa msimu, amekuwa gumzo, akipendekezwa kuchukua mikoba ya Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal (Sunday Express)
Hata hivyo, West Ham wanamhitaji Emery achukue mikoba ya David Moyes. Meneja wa zamani wa Manchester City Manuel Pellegrini na meneja wa zamani wa Watford Marco Silva wanamtamani Emery.(Sun on Sunday)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, anataka kitita cha pauni milioni 200 kama atakuwa meneja wa Arsenal.(Sun on Sunday)
Manchester City inataka saini ya kiungo wa kati wa Napoli,Jorginho, 26, na mshambuliaji wa pembeni Riyad Mahrez, 27, wa Leicester kwa gharama ya takriban pauni milioni 110 (Mail on Sunday)
0 maoni: