![]() |
Advertisement |
Klabu ya soka ya Mtibwa sugar yenye maskani yake Manungu Tuliani Morogoro leo imeibuka kidedea Mara baada ya kuichapa bao 3 bila majibu klabu ya soka ya Buseresere yenye makao yake Mkoani Mwanza katika michuano ya Azam sports Federation cup
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa nyamagana ilemela jijini Mwanza mbaka dakika 45 za kwanza kumalizika hakuna klabu iliyokuwa imeona lango La mwenzie
Kipindi cha pili klabu ya Mtibwa sugar ilianza kuonyesha mashambulizi yake na kupata goli la kwanza dakika ya 53 likipachikwa kimyani na mchezaji hassani dilunga.
Kasi ya mchezo iliendelea Mtibwa sugar wakafanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa mchezaji wao Chanongo dakika ya 83 huku mchezaji Makalani akihitimisha idadi ya magoli katika mchezo huo kwa kuiongezea Mtibwa sugar bao la 3 na mchezo huo kuisha kwa Mtibwa sugar kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli tatu kwa bila
Mtibwa sugar inakuwa timu nyingine inaopanda hatua inayofuata katika michuano hii Mara baada ya Njombe mji kupanda mwanzoni Mwa wiki hii
Mchezo mwingine naosubiriwa kwa hamu ni kati ya yanga na Majimaji utakaochezwa katika uwanja wa majimaji mjini Songea Mchezo huu utahitaji timu moja itakayoungana na Mtibwa sugar na njombe mji katika hatua inayofuataa
0 maoni: