Jumanne, 10 Aprili 2018

Zesco wamtangaza lwandamina kuwa kocha wao

ad300
Advertisement

Mabingwa wa Zambia, Zesco wamemtangaza rasmi kocha George Lwandamina kuwa kocha wao mpya.
Lwandamina ambaye bado ana mkataba na Yanga, ameondoka bila ya kuaga na Yanga hawakuwa wakijua alipo.
Lakini Kocha huyo, ametangazwa leo rasmi kurejea kwa Zambia na kujiunga na klabu yake hiyo ambayo aliiacha na kujiunga na Yanga.
Mabingwa hao wa Zambia, wamesema wameishamalizana na Lwandamina na ataanza kazi mwezi ujao.
Aliyekuwa Kocha wa Zesco, Tenant Chembo aliamua kuachia ngazi na Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, Richard Mulenga anaonekana ndiye alifanya juu chini kuhakikisha Lwandamina anarejea.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo jioni, Zesco imesema imeamua kumrejesha Lwandamina kutokana na ubora na weledi wake kwa lengo la kuendelea kuijenga zaidi kwa upande wa wachezaji na kuboresha umoja kati ya uongoza, wanachama na mashabiki wao.
Wakati kocha mkuu amejiuzulu, msaidizi wake Emmanuel Siwale ndiye ataiongoza Zesco kesho dhidi ya Lusaka Dynamo

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: