Jumatano, 11 Aprili 2018

Wanaharakati waeleza Mazito juu ya zoezi linaloendeshwa na Makonda

ad300
Advertisement

Kufuatia zoezi linaloendeshwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam la kuwasikikiza na kutetea wanawake waliotelekezwa na wanaume bila kupata msaada na maisha  yao na watoto wao bado hayaridhishi wanaharakati nchini wametofautiana juu ya utaratibu huo unaoendeshwa chini ya ofisi  ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwasikiliza na kuwapa ushauri wa kisheria wanawake wenye watoto ‘waliotelekezwa’ na waume zao.

Wanaharakati hao wameeleza kuwa jambo hilo licha ya uzuri wake, lina kasoro.

Wakizungumza na  na kituo cha habari cha MCL Digital leo Jumatano Aprili 11, 2018, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Tike Mwambipile amesema kitendo cha watoto hao kupigwa picha na kuonyeshwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Amesema hata wanaofanya kazi ya kusikiliza wanawake waliotelekezwa kwa siku husikiliza zaidi ya wanawake 30, lakini hawafanyi matangazo kama ilivyo kwa hao wanaosikilizwa katika ofisi ya mkuu huyo wa mkoa iliyopo wilyani Ilala jijini hapa.

Amebainisha kuwa lazima utu wa mama na mtoto kuheshimiwa, "ndio maana habari za watoto haziruhusiwi kuripotiwa maana ni mambo ya usiri.”

Amesema hatua iliyofanywa na kiongozi huyo ni nzuri kwa kuwa inaonyesha ukubwa wa tatizo katika jamii, kwamba mashirika yanayoshughulikia masuala ya wanawake yanapaswa kuweka nguvu ya pamoja na kutoa elimu.

Mkurugenzi wa Shirika la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita amesema tatizo analoliona katika jambo hilo ni suala zima la sera za nchi kusimamiwa kivitendo ili kuweza kumsaidia mwanamke na mtoto.

Amesema wizara inayosimamia afya ina jukumu kubwa la kuhakikisha mtoto anapatiwa huduma mbalimbali ikiwemo bima ya afya kwa maelezo kuwa kama wanawake wamefika kwa mkuu huyo wa mkoa na tatizo lao kutangazwa katika vyombo vya habari hautakuwa msaada kwao.

“Mama mpaka katoka nyumbani kafika pale ina maana ana matumaini ya kutafutiwa suluhu ya tatizo lake, ni vyema Serikali ikahakikisha inamfutilia mpaka mwisho kuona kweli haki za mtoto zilizokiukwa zinatekelezwa ikiwemo suala zima la huduma za afya,"amesema.

Mkurugenzi chama cha Wajane (TAWIA), Rose Serwati amesema utaratibu huo wa Makonda unaweza kuchangia kuvunja ndoa na kuweka uadui kati ya baba, mama na mtoto.

"Unajua wanaume wengi hawapendi kulazimishwa kufanya jambo fulani, sasa unapokuwa umemunyesha  kwenye vyombo vya habari na mwanamke kumlaumu kuna hasira wanaijenga mioyoni mwao,” amesema.

“Baba huyu anaweza kujikuta anaishia kutuma hela kwa mtandao wa simu kama njia ya kutimiza majukumu yake lakini hana mpango wa kumuona mtoto …, wengine ni waume za watu ambao huwezi kujua pengine walikuwa katika kuzipanga familia zao kwanza ili kuweza kumtambulisha mtoto aliyemzaa nje ya ndoa.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: