Alhamisi, 19 Aprili 2018

Addo shaibu "Hoja za ccm ni dhaifu sana"

ad300
Advertisement

Bunge Liagize Uchunguzi Maalum Juu ya Matumizi ya Shilingi Trilioni 1.5 za Watanzania. Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema hayo leo Alhamisi Aprili 19, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ufafanuzi wa kauli  na hoja zilizosemwa na CCM jana. Aidha ameeleza kuwa chama cha ACT wazalendo kimeshaandika barua kwa spika kuomba bunge lifanye uchunguzi wa fedhaTrillion 1.5 ambazo hazijajulikana matumizi yake kwa mujibu wa ripoti ya CAG.

Akijibu hoja  za ccm xilizotolewa na Hamphrey polepole Addo shaibu Amesema kuwa hoja ya kwamba ACTwazalendo ni chama kidogo, chenye mbunge mmoja, hivyo hakina uwezo wa kufanya uchambuzi wa ripoti ya CAG.  Ni hoja dhaifu yenye kutaka kututoa kwenye mstari

"Hoja hii ni dhaifu, ni dhihaka ya kututoa kwenye mstari, maana pia haelezi kuwa ili chama cha siasa kichambue kinapaswa kiwe na ukubwa kgani na kiwe na wabunge wangapi, na hasemi kwamba masharti hayo anayoyaweka ni kwa mujibu wa sheria gani ya nchi?

Uchambuzi wa ni suala kitaalam, halina uhusiano na udogo au ukubwa wa chama, au idadi ya wabunge wake. Ili Mtu, au Chama cha Siasa afanye uchambuzi wa ripoti ya CAG, yanahitajika mambo matatu muhimu:

Mosi ni Weledi (Proffesionalism), Pili ni Ujuzi (Skills), na tatu ni Uzoefu katika eneo husika (Experience). Hivyo uchambuzi wa ripoti hii si zao la ukubwa wa chama wala idadi ya wabunge"

Aidha Addo shaibu ameeleza kuwa hawana mashaka na kiwango cha weredi cha mbunge Zitto zuberi kabwe kama kiongozi mkuu wa chama na alliyeongoza uchambuzi wa chama kahusu ripoti ya CAG

zitto kabwe, ambaye aliongoza timu iliyofanya uchambuzi wetu juu ya  ripoti ya CAG 2016_17, ni Mchumi Mweledi kitaaluma, ana Ujuzi wa kutosha juu ya masuala ya Uchumi na Ukaguzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali nchini na vya nje ya nchi.

Na ana uzoefu wa kuchambua taarifa za CAG kwa kuwa ameongoza Kamati za Bunge za POAC na PAC kwa miaka hiyo 8. Sifa zote hizo zinatupa hadhi na heshima stahili sisi ACTwazalendo, pamoja na kuwa chama kidogo tu chenye mbunge mmoja, kufanya uchambuzi wa ripoti ya CAG

Aidha ACT wazalendo wameeleza kufurahishwa na mapokeo ya watanzania katika uchambuzi walioufanya kwenye ripoti ya CAG

"Aprili 15, 2018, ACTwazalendo tulifanya uchambuzi wa awali wa ripoti ya CAG Tunafurahi kuwa uchambuzi wetu juu ya masuala 8 ya hatari kwenye taarifa ya CAG umepokelewa vyema, na umekuwa ni mjadala wa kitaifa."



Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: