Alhamisi, 19 Aprili 2018

Nandy, Diamond wawasili TCRA

ad300
Advertisement

Wasanii wa bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’na Faustina Charles ‘Nandy’ wamewasili katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Wasanii hao wanaitikia wito wa TCRA ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa video zao zinazokiuka maadili.

Nandy aliwasili TCRA saa 5:48 asubuhi leo Aprili 19 na Diamond aliwasili saa 6:15 mchana. Diamond alisindikizwa na menejimenti yake ikiongozwa na Said Fella.

Hivi karibuni, Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe alizungumza bungeni kuwa wasanii hao walikamatwa na kuhojiwa kuhusu kusambaa kwa video zinazokiuka maadili.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alithibitisha kuwahoji wasanii hao.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: