![]() |
Advertisement |
Chama cha ACT wazalendo kimesema kuwa kitaendelea kuitaka Idara ya usalama wa Taifa (TISS) Kujitathimini na kwamba mageuzi yanahitajika katika utendaji kazi wa chombo hicho na kurejesha hadhi ya chombo hicho
akizungumza na wanahabari hii leo kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema kuwa
"TISS si usalama wa CCM wala serikali.Yanapotokea matukio makubwa yanayotishia usalama wa taifa letu,Mkurugenzi anapaswa kuwajibika"
Pia akigusia suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji Zitto kabwe amesema kuwa baada ya kupatikana kwa Mohammed Dewji kama taifa bado lina jukumu kubwa la kuhakikisha hao ambao hawajapatikana wanapatikana wakiwa hai au kama hawako hai ndugu zao wapewe nafasi ya kuifanya dua na sala.
Katika hatua nyingine chama cha ACT wazalendo kimeitaka serikalii iwajibike katika sakata la korosho na kusema kuwa kulikua na ulanguzi mkubwa wa salfa ,na mkulima alinunua dawa shilingi 84,000 kutoka shilingi 14,000 iwapo fedha za Ushuru wa Korosho (exports levy) zingetumika kama ilivyopaswa na Serikali isingezidhulumu."
Lakini pia chama hicho kimeishauri serikalii kuongeza kasi ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho nchini ili kuongeza thamani ya korosho yake badala ya kuendelea kusafirisha korosho ghafi
Vile vile chama hicho kimeitaka serikalii kununua korosho za wakulima kwa bri ya mwaka jana ya shillingi 4000 ili yenyewe(serikalii) iwauzie wenye minada ili kuepusha hasara kwa mkulima
Pia Chama cha ACT kimemtaka Rais aombe radhi kwa wabunge waliokuwa wakitetea zao la Korosho kutokana na kauli yake ya kuwatisha kiasi cha kusema angeanza kwa kupiga mashangazi zao. Zitto Kabwe amesema kuwa
"Tunamtaka Rais Magufuli awaombe radhi wabunge wa kusini ambao aliwadhihaki wakati wanapigania fedha za export levy ambazo zingesaidia kuinua zao la korosho nchini, kuomba radhi ni uungwana"
Lakini pia Zitto Kabwe ameitaka serikali kuongoza nchi kwa maarifa na si kwa mabavu
"Tunarudia Rai yetu ya mara zote kuwa kuongoza ni maarifa, si mabavu. Serikali iwe tayari kupokea mawazo chanya kwa ustawi wa taifa letu. Tanzania ni yetu sote"
Katika hatua nyingine chama cha Act wazalendo kimetangaza kutoshiriki katika chaguzi za marudio kutokana na kutoridhishwa na hali ya kisiasa hapa nchini.
0 maoni: