Alhamisi, 11 Oktoba 2018

JE MO DEWJI NI NANI..?

ad300
Advertisement

Mo alizaliwa tarehe 8 Mei mwaka 1975, ikiwa na maana kwamba kwa sasa ana miaka 43.

Alizaliwa eneo la Ipembe, Singida maeneo ya katikati mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes, ana utajiri wa dola bilioni 1.5

Ni wa pili miongoni mwa watoto sita wa Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji.

Alisomea elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Arusha na baadaye akasomea elimu ya sekondari katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.

Alihamishiwa Marekani kwa masomo zaidi ya sekondari katika jimbo la Florida mwaka 1992.

Alisomea chuo kikuu cha Gerogetown jijini Washington DC na kuhitimu mwaka 1998 akiwa na shahada ya kwanza katika biashara ya kimataifa na fedha, na masuala pia ya dini. Miongoni mwa watu mashuhuri waliosomea chuo kikuu hicho ni rais Bill Clinton, rais wa zamani wa Ufilipino Gloria Arroyo, Mfalme wa Jordan Abdullah na wachezaji wa NBA kama vile Allen Iverson na Patrick Ewing.

Baada ya kufuzu, alirejea Tanzania na kuanza kushiriki katika usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.

Fedha
Image captionFedha

Alihudumu kwa miaka miwili kabla ya kuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, wadhifa ambao ameendelea kuushikilia hadi sasa.

Mo ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia miongoni mwa matajiri wa umri mdogo zaidi Afrika.

Kampuni ya METL, kwa mujibu wa Forbes, ilifanikiwa kwa kununua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa.

METL ina viwanda vya kutengeneza nguo na  bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.

Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.

Kwa mujibu wa tovuti yake, METL inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.

Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

METL ina shughuli zake katika nyingi barani Afrika na ina malengo ya kujipanua zaidi katika maeneo zaidi.

Inaendesha shughuli zake Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji na Zambia, ambapo huajiri watu zaidi ya 28,000.

Image copyrightAFPMo Dewji

Shughuli za MeTL huchagia 3.5% ya jumla ya pato la taifa (GDP) la Tanzania.

Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2014 kutoka $30 milioni hadi $1.3 bilioni kilikuwa ni 200%.

Lengo la kampuni hiyo ni kuongeza mapato ya taifa lake hadi $5bn kufikia mwaka 2020, pamoja na kuwaajiri watu 100,000.

Mo Dewji ameorodheshwa wa 17 kwenye orodha ya mabilionea barani Afrika na wa 1561 duniani kwenye orodha ya mabilionea mwaka 2018.

Wakati mmoja kampuni yake ilianzisha Mo Cola kushindana na Coca Cola.


Dewji ni Mtanzania pekee aliyesaini mkataba mwaka 2016 wa kutoa kwa wahitaji nusu ya mali yake.

Mo Dewji Foundation ndio asasi ambayo aliianzisha mwaka 2014 ili kutekeleza nia yake hiyo na kazi yake kubwa ni kusaidia watanzania wasiojiweza kwa upande wa afya, elimu na maendeleo jamii.

Mbali na biashara na shughuli za jamii Mo Dewji amewahi kuwa mwanasiasa na mwaka 2005 mpaka 2015, Mohamed Dewji alikuwa mbunge wa Singida Mjini.

Alijiingiza katika siasa mara ya kwanza mwaka 2000 ambapo alishinda uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo, wakati huo akiwa na miaka 25, lakini akazuiwa kuwania kwa madai kwamba alikuwa bado mdogo wa umri.

Alistaafu kutoka kwenye siasa baada ya kuhudumu mihula miwili.

Mwaka 2012, alitawazwa Kiongozi Mdogo Duniani kwa Kiingereza Young Global Leader (YGL) wakati wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa uchumi Duniani (WEF).

Mwaka 2015, alitajwa kuwa bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika na jarida la Forbes na baadaye akatawazwa Mtu Mashuhuri wa Mwaka wa Forbes.

Mwaka uliopita, alishinda tuzo ya Afisa Mkuu Mtendaji bora wa Mwaka Afrika katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu watendaji wa Afrika.


Mke wa Dewji huitwa Saira, aliyekuwa wanapendana tangu utotoni, na wamejaliwa watoto watatu Nyla, Abbas na Mahdi. Alifunga ndoa mwaka 2001. Mo na mke wake walikutana Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.


Dewji pia ni mpenzi wa michezo na amewekeza katika klabu ya mpira ya Simba inayocheza katika Ligi Kuu ya Tanzania ambapo ni mfadhili mkuu kwa sasa.

Amekuwa akifadhili ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: