![]() |
Advertisement |
Mbunge wa kigoma kupitia chama cha ACT wazalendo mheshimiwa Zitto zuberi Kabwe ameonesha wasiwasi mkubwa kwenye usimamizi wa fedha za serikali na kueleza kuwa fedha za umma haziko salama kufuatia ripoti iliyotolewa na mkaguzi wa hesabu za serikali CAG ambapo katika ripoti hiyo iliyotolewa wiki hii serikali kuu ya Tanzania ilipata hati chafu kupitia kurasa ya Facebook na tweeter zitto kabwe ameeleza kuwa
"Serikali Kuu ( Hesabu Jumuifu za Taifa ) imepata HATI CHAFU. Sababu za Hati Chafu kwenye Sura ya Nne na ya Tano ya Taarifa ya CAG zinatishia kabisa uwa Fedha za Umma. Kesho nitazungumza na Waandishi wa Habari kuchambua Taarifa ya CAG ya mwaka 2016/17 na kufafanua hoja nzito sana alizotoa CAG kwenye ukaguzi wake kwa Serikali Kuu. Kiufupi Fedha za Umma hazipo salama chini ya Utawala wa Awamu Tano iwapo wataendelea na mtindo wa Uongozi walio nao. Kuanzia saa tano kamili asbh tutakuwa livestream pia kwenye akaunti hii"
0 maoni: