Jumamosi, 14 Aprili 2018

Harusi ya Kiba yawadia na sasa Mambo ni Motoo..!

ad300
Advertisement

Kenya.Mashabiki wa mkali wa Bongo Flava, Ali Kiba waliamini kabisa mrembo Jokate Mwegelo ndiye angekuwa mke halali wa supastaa huyo, lakini mambo yamekuwa tofauti.
Habari za kuaminika ni kuwa, Kiba anatarajiwa kufunga ndoa na mpenzi wake Amina Khaleef, Alhamisi ijayo mjini Mombasa.
Ndoa ya Kiba na Khaleef ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki, ambapo sasa mambo ndio yamekuwa moto huku amsha amsha za harusi hiyo zikipamba moto.
Imeelezwa kuwa, mpango mzima wa harusi hiyo unasimamiwa na rafiki wa karibu na Kiba, Sultan Joho ambaye ni Gavana wa kaunti ya Mombasa.
Kwa sasa Kiba yuko nchini China ambako amekwenda kukamilisha baadhi ya mambo ikiwemo kununua samani za nyumba yake iliyopo maeneo Tabata, Dar es Salaam.
“Kila kitu kinakwenda vizuri, ndoa hii itafanyika hapa Mombasa na nyingine kule Dar es Salaam. Kwa sasa Kiba yuko nchini China kukamilisha mambo madogo madogo ya nyumbani, lakini hapendi habari za hii ndoa kujulikana.
“Ndoa itafungwa Aprili 19 hapa Mombasa na kule Dar itakuwa Aprili 29, shughuli nzima inasimamiwa na marafiki zake wa karibu akiwemo Joho (Sultan),” kilisema chanzo chetu.
Hivi karibuni mkali mwingine wa Bongo Flava, Ambwene Yesaya a.k.a AY alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku, ambapo alifanya sherehe mbili moja kule Kenya na nyingine hapa Tanzania.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: