![]() |
| Advertisement |
Msanii wa vichekesho nchini Kenya Eriki omondi ameomba msamaha mashabiki zake kufuatia video iliyokuwa ikimuonesha akiogelea na watoto huku akiwa hajajisitiri.na akiwa mtupu wakenya wengine wameonesha kukasirishwa na kitendo hicho wengi wakitafsiri kuwa ni unyanyasaji dhidi ya watoto
Lakini Eric omondi anasema ilikuwa ni Comedy tu na hakuwa na mpango wa kukera watu.
Akizungumza na eDaily Mr.Omondi amesema kuwa lengo lilikuwa ni kuzungumza kuhusu utamanduni wa Waafrika na pia maisha ya watu waishio vijijini ni hivyo tu.. na sikudhani kwamba aliyechukua video ataiweka katika mitandao ya kijamii.
Nimetafakari. Juu ya kile nilichokifanya nimegundua kuwa nilichofanya hakikuwa sahihi niwe tu mkweli nilichofanya ni kibaya tena kibaya sana nataka kuzungumza hilo kutoka ndani ya moyo wangu samahani kwa wote walioathiriwa na kitendo nilichofanya kwa wakenya na wengine nje ya Kenya.
Lakini pia kupitia ukurasa wake ya Instagram Eriki Omondi ameandika.
Nimekuwa mchekeshaji maisha yangu yote, nimekosea mara nyingi sana, leo ilikuwa miongoni mwa siku nilizo kosea sana, nimewakera wengi ila halikuwa thumuni langu kufanya hivyo, NAOMBA RADHI SANA KWA HILO JAMBO".
I have been a comedian all my life... Many are the times that I have errored... Today was one of those days. I have offended so many. I did not in any way intend to offend anyone...I AM DEEPLY SORRY FOR THAT... 🙇♂️


0 maoni: