![]() |
Advertisement |
Klabu ya soka ya Chelsea imepata ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Klabu ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu
Chelsea inafikisha alama 60 baada ya michezo 33 na kubaki nafasi ya 5 huku Southampton ikibaki na alama 28 katika nafasi ya 18 na taarifa nyingine kutoka EPL ni kwamba
Kevin De Bruyne(Manchester City) na Mohamed Salah(Liverpool) wanatarajiwa kuchuana vikali kuwania tuzo ya mchezaji bora katika ligi ya mpira wa soka baada ya kutajwa katika orodha ya wachezaji 6 wanaowania tuzo hiyo
Wachezaji wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Harry Kane(Tottenham), Leroy Sane(Manchester City), David De Gea(Manchester United) na David Silva(Manchester City)
Eden Hazard(Chelsea), Roberto Firmino(Liverpool) na Raheem Sterling(Manchester City) ni miongoni mwa majina makubwa katika ligi hiyo ambayo hayajatajwa kuwania tuzo hiyo
De Bruyne mpaka sasa amefunga magoli 7 na kutoa pasi zilizozaa magoli 15 katika michezo 32 ya ligi hiyo.
Salah mpaka sasa ni kinara wa magoli katika ligi hiyo akiwa na magoli 29
0 maoni: