![]() |
Advertisement |
Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole amedai kuwa kuna viongozi wa vyama vya siasa wanapotosha ripoti ya CAG na inafaa uwekwe utaratibu waanze kuchukuliwa hatua
Polepole amesema kuna kiongozi mmoja wa upinzani amekuwa akizungumza uwongo na kuleta taharuki kwa wananchi na kusema inafaa achukuliwe hatua ili aache
Polepole amesema hayo leo Jumatano Aprili 18 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG).
Polepole amesema, “Huyu ni muongo alianza na santuri ya njaa akatangaza nchi ina njaa. Tumezunguka nchi nzima hakuna njaa, akaona haitoshi akamgeukia rais wetu kuwa ni dikteta wakati yeye anaendesha chama kupitia Facebook.”
“Kuna wakati anasema kamati kuu imekaa kumbe uongo anaandika facebook”
“Niombe uongozi wa Bunge wakati mwingine uwe unawabana wabunge wawe wanathibitisha mambo wanayoyazungumza bungeni.”
“Wenye dhamana ya kusimamia sheria wachukue hatua, kucheka cheka na mizaha kwa kauli hizi haivumiliki. Tunataka aeleze hiyo Sh 1.5 trilioni kaipata wapi, alizua taharuki, nasisitiza tusimuache alizoeshwa vibaya huyu maana tunajua sisi ndio tupo kwenye chama.”
Polepole amesema anaipongeza serikali ya CCM kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuweka hadharani ripoti ya CAG na kuchukua hatua kwa wanaofanya ubadhirifu unaobainishwa
Polepole anaipongeza serikali kwa kuwa Rias Magufuli alipochukua hatua za awali, mawaziri nao walifuta hatua hizo na kuwachukulia hatua maafisa kwenye wizara zao
Polepole amesema pia vipo vyama vya siasa vinatumia fedha ya umma na havitoi hesabu na kusemainabidi vichukuliwe hatua kali za kinidhamu
Amesema vipo vyama vimetumia zaidi ya Sh. milioni 700 bila kutoa hesabu, pia vipo vyma ambavyo vinatumia fedha bila kufuata kanuni za kihasibu
Kuna chama kinaitwa ABC, SAU,
CHADEMA wametumia fedha bila kutoa hesabu zilivyotumika na pia kutumia fedha zaidi ya bilioni 2.2 bila kupeleka benki na kuhoji vinawezaje kuikosoa serikali?
Pia CHADEMA imefanya manunuzi ya zaidi ya bilioni 24 bila kushindanisha wakati ndio hao wanaoisema serikali
Polepole anasema isiidhie kuwataja kwenye taarifa ila msajili achukue hatua, hata kama ni ndani ya CCM
Polepole amesema inapotoshwa kuwa CCM imekopa ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii, CCM ina utaratibu wake wa ndani wa kulinda maslahi ya watumishi wake tofauti na vyama vingine
CCM ina utaratibu wa kulimbikiza fedha kila mwisho wa mwezi ili watumishi wake wanapomaliza utumishi, ipo fedha ya kuwalipa mafao yao
Katika akaunti ya CCM inayosimamiwa na Baraza la wadhamini walitoa zaidi ya milioni 300 ili watumishi wanaaondoka walipwe na wanazirudisha ili mfuko uendelee kunona
Amesema CHADEMA wamepotosha juu ya hili na wanapaswa kuchukuliwa hatua
Polepole pia anasema serikali ya CCM sasa ina utaratibu wa kuweka hesabu za serikali katika mtindo jumuishi, zamani zilikuwa zikitolewa kwa wizara na taasisi moja moja lakini kwa sasa unaweza kuzipata katika sehemu moja
Tanzania ni nchi ya pekee kufanya hivyo katika Afrika Mashariki na hii inasaidia kuweka mambo wazi zaidi na mtindo huu ni mgumu
Polepole amesema Zitto Kabwe ndio anaongoza kupotosha ripoti ya CAG kwa kukurupuka naripoti asizozielewa, na kusema Taarifa ya CAG ilikuwa imeshapitiwa na wao kwanza
Polepole anasema anapotosha kuwa trilioni 1.5 zimepotea na kufafanua kuwa sasa kuna mtindo mpya ambao unafuata vigezo vya kimataifa vya ukaguzi wa hesabu za umma unaitaka serikali inapokagua fedha zake zinapoingia kuhesabu pia na pesa baada ya serikali kuwa imetoa huduma ,
zamani ilikuwa ni lzaima ipokee fedha kwanza ndipo ihesabu fedha imeingia, ila sasa huduma inapotolewa hata kama fedha haijakusanywa inahesabiwa (acrrual basis)
Makusanyo ghafi ni makusanyo ya jumla, baada ya makusanyo ghafi inatakiwa ukokotoe ujue makusanyo sahihi ni yapi
Tumekusanya trilioni 25.3, pesa ambayo huduma imetolewa na inatarajiwa imekushwa kuingizwa kwenye jumla hiyo
ukitaka kujua makusanyo halisi unachukua trilioni 25.3 unatoa makusanyo tarajiwa (receivables)
Unachukua trilioni 25.3 unatoa bilioni 687.3 (receivables) kama hatua kupata makusanyo halisi
Pia unatoa bilioni 203.92 ambazo ni fedha zilizokusanywa kwa ajili ya Zanzibar, ambayo haisomwi kwenye bajeti ya Serikali ya Muungano
Ukitoa hesabu hizo unapata Shilingi trilioni 24.4 hizi ndio makusanyo halisi ya mwaka 2017/208
Zitto anadai pesa zilizotumiaka kutoka trilioni 25.3 ni trilioni 23.79, hii kipindi mkaguzi anapita zilikuwepo fedha za serikali ambazo zilikuwa kwenye hatifungani (zilikuwa hazijaiva) ambayo ni shilingi 697.85 bilioni
Ukichukua 697.85 bilioni ukijumlisha trilioni 23.5 unapata trilioni 24.4, na ukichukua 25.3 ukatoa 23.79 unapata 1.5 trilioni ambayo ndio zitto anadai imeibiwa
Polepole anasema Zitto hajui hesabu na anapaswa kumtafuta mwalimu
Polepole anasema pia Zitto amepotosha kuhusu bilioni 219 ambayo ililipa madeni ya zamni ambayo hayakuwa yamepitishwa na Bunge
Amesema haesabu za serikali zinawekwa kwenye vifungu, na kulikuwa na madeni ya watu mbalimbali yanayofikia bilioni 969 ambayo yalipitishwa na Bunge na serikali inayalipa baada ya kuyahakiki, bilioni 219 ni sehemu ya bilioni hizo 969 zinazofahamika na Bunge pia
0 maoni: