![]() |
Advertisement |
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsaini kiungo wa kati Mbrazil Fred kutoka Shakhtar Donetsk ili kujaza nafasi inayoachwa na mchezaji Paul Pogba.
Real Madrid inahitaji kumpata mchezaji wa kimataifa Mfaransa paul pogba lakini rais wa timu hiyo Florentino Perez hawezi kusaini mchezaji mwenye Umri kuanzia miaka 25.Labda apunguze mahitaji yake ya mshahara na aoneshe kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Dunia. (Express)
Manchester City inampango wa kumpata mshambuliaji wa Ufaransa anaekipiga katika klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 19, na kiungo wa Bayern Munich, Thiago Alcantara Mwenye umri we miaka 27 na wote wanatarajiwa kutua Etihad msimu huu. ( Skyports)
Mchezaji wa Uingereza anayecheza katika klabu ya Norwich, James Maddison, mwenye umri wa miaka 21, anahitajika na vilabu kadhaa vya Ligi Kuu, ikiwa ni pamoja na Tottenham, Arsenal, Everton na Manchester City. (Telegraph)
Borussia Dortmund anataka kupata saini ya mchezaji Michy Batshuayi kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea, wakati wa majira ya joto. Chelsea inataka zaidi ya £ 50m kwa mchezaji huyo wa ubelgiji mwenye umri wa miaka 24.
Chelsea inataka kumsaini mchezaji wa Nice Jean Michael Seri kwa ada ya £ 35m, lakini mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kusubiri na kuona ni nani atakuwa mmiliki wa the Blues msimu ujao. (Mirror)
Luke Shaw bado hajafanya uamuzi kuhusu maisha yake ya baadaye huko Manchester United. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ataamua hatima yake mwishoni mwa msimu, baada ya kuwa na uhusiano mgumu na meneja wa manchester united Jose Mourinho. (ESPN)
Barcelona inahitaji kuwa na hadi £ 60m ili kumpata mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial mwenye umri wa miaka 22, na Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 17 kutoka Fulham. imeeleza klabu hiyo kupitia email yake
Liverpool na Tottenham walikuwa miongoni mwa timu pande zote za Ligi Kuu ya Uingereza zilizotuma waangalizi wake kumtazama winger wa Benfica kutoka nchini Serbia na Andrija Zivkovic katika mchezo wa Premier ligi dhidi ya Porto. (The sun)
0 maoni: