Jumatano, 18 Aprili 2018

Zitto kabwe "Niko tayari kufa"

ad300
Advertisement

Mbunge wa kigoma mjini kupitia tiketi ya chama cha ACT wazalendo amemjibu mkuu wa itikadi na uenezi  wa chama cha mapinduzi ccm Hamphrey polepole na kusema kuwa yuko tayari kukamatwa  kupitia mtandao wake wa  Facebook Zitto ameandika

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG.

Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO.

Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa).

Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"

Hatua hii imekuja kufuatia mkutano alioufanya Hamphrey polepole na waandishi wa  habari na kusema kudai kuwa Zitto kabwe ni mbunge anayepotosha umma kuhusu fedha Tillioni 1.5 ambazo hazijulikani zilipo kwa mujibu wa ripoti ya CAG katika mkutano huo polepole alieleza kuwa mbunge Zitto anapaswa kukamatwa na kulishauri bunge kuwachukulia hatua watu wanaopotosha umma

Hivi karibuni Zitto kabwe alifanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa serikali inapaswa kutolea majibu maswali yaliyoulizwa na CAG huku akipinga utaratibu wa mawaziri kujibu maswali hayo kupitia mikutano na waandishi wa habari .Jambo ambalo Bunge lilifafanua na kuweka wazi kuwa halina madhara kisheria na majibu rasmi yatawasilishwa bungeni kwa utaratibu unaohusika

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: