Jumatano, 11 Aprili 2018

Kesi ya ukomo wa madaraka yaanza kusikilizwa

ad300
Advertisement

Mbale, Uganda. Jopo la majaji watano wa Mahakama Kuu, Jumanne lilianza kusikiliza kesi ya kupinga marekebisho ya Katiba kwa kufuta Ibara ya 102(b) iliyolenga kuondoa ukomo wa umri wa rais.

Majaji waliomo kwenye jopo hilo ni Naibu Jaji mkuu Alfonse Owiny-Dollo, pamoja na Remmy Kasule, Elizabeth Kibuuka Musoke, Cheborion Barishaki na Kenneth Kakuru.

Desemba 20, 2017, Bunge lilipitisha Sheria ya Marekebisho ya Katiba mwaka 2017 ambayo iliondoa ukomo wa umri wa rais uliokuwa umebainishwa katika Ibara ya 102(b) ya Katiba. Katika marekebisho hayo, pia Bunge lilirejesha ukomo wa umri kwa viongozi wa serikali za mitaa uliokuwa umeondolewa Septemba 2005 na likaongeza muhula wa Rais na Bunge kutoka miaka mitano hadi saba.

Marekebisho hayo ilikuwa mwisho wa mjadala uliodumu kwa miezi mitatu uliosababisha vurugu ndani ya Bunge ikiwemo hatua ya walinzi wa usalama kuingia ndani na kuwatoa wabunge waliokuwa wamesimamishwa kwa kile Spika Rebecca Kadaga alichoita utovu wa nidhamu. Ni kutokana na mazingira haya marekebisho hayo yanapingwa mahakamani.

Jumanne, majaji watano wa Mahakama ya Katiba wanaosikiliza kesi hiyo ya ukomo wa umri wa rais katika Mahakama Kuu ya Mbale walishangaa na kuwahoji walalamikaji ni kwa namna gani Spika wa Bunge Rebecca Kadaga angeweza kupitisha sheria ambayo yeye binafsi aliona kasoro katika mchakato wake.

Kutokana na swali hilo, majaji waliwapa jukumu wanasheria wa warufani kuliongoza jopo kwa ushahidi utakaoonyesha kasoro za kikatiba ambazo Spika anaweza kuwa hakuzitazama wakati muswada ulipowasilishwa ndani ya Bunge.

Wanasheria hao waliambatanisha ushahidi kwa kunukuu kitabu cha kumbukumbuka za mchakato wa Bunge Hansard kutoka Septemba 27, 2017 hadi Desemba 19, 2017 kipindi ambacho muswada uliwasilishwa bungeni hadi uliposomwa kwa mara ya pili.

Ushahidi uliomo kwenye vitabu vya Hansards unaonyesha kwamba Spika, katika nyakati mbili tofauti, alimkosoa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Jacob Oboth -Oboth, kwa kuhusisha muda wa wabunge kukaa ofisini, wakati hilo halikuwa moja ya masuala ambayo aliwasilisha kwenye kamati hiyo ili yajadiliwe.

 

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: