Ijumaa, 2 Machi 2018

Wabunge 13 kufunguliwa kesi Mahakamani

ad300
Advertisement

Hivi karibuni Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alihukumiwa kifungo cha miezi 5 jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kumkuta na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais Dkt Magufuli.

Katika kesi hiyo, Sugu alihukumiwa pamoja na Katibu wa CHADEMA Nyanda za Juu Kusini ambapo alikuwa mbunge wa pili wa CHADEMA kuswekwa gerezani akitanguliwa na Peter Lijua Likali ambaye Januari 11, 2017 yeye na dereva wake walihukumiwa kifungo cha miezi 6 jela, lakini mahakama ikamuachia huru Machi 31.

Mbali na hao, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema mpaka sasa wabunge 13 wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini wanakabiliwa na kesi katika mahakama mbalimbali nchini.

Aliwataja wabunge hao kuwa ni Godbless Lema (Arusha Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Peter Lijualikali(Kilombero), Susan Kiwanga (Mlimba) na Zubeda Sakuru wa viti maalumu.

Wengine ni Pascal Haonga (Mbozi), Halima Mdee (Kawe), Frank Mwakajoka (Tunduma), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Kunti Yusuph (Viti Maalumu), Cecil Mwambe (Ndanda) na Saed Kubenea wa Ubungo.

Lissu, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Ubelgiji anakabiliwa na kesi zaidi ya tatu za uchochezi.

Lema anakabiliwa na kesi ya uchochezi ambayo ilimfanya kuwekwa mahabusu kwa siku 121 baada ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali kuweka zuio la dhamana huku Mdee akikabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi pia.

Wengine wenye kesi za uchochezi au kuikashfu Serikali au viongozi waliopo madarakani ni Haonga na Mwakajoka.
Mchungaji Msigwa anakabiliwa na kesi kadhaa ikiwamo ya hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa akishtakiwa kwa kesi mbili. Mbunge huyo ni mshtakiwa wa saba katika kesi hizo, moja anadaiwa kuchoma moto nyumba ya Mary Tesha aliyokuwa akiishi Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Alphonce Muyinga na ya pili, mbunge huyo na wenzake sita wanadaiwa kupanga njama ya kutenda uhalifu kinyume cha sheria

Kwa upande wao, Lijualikali, Kiwanga na wanachama 34 wa Chadema mkoani Morogoro wanatuhumiwa kwa makosa manane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata Sofi iliyopo wilaya ya Malinyi.
Comments SIASA

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: