![]() |
| Advertisement |
Klabu ya simba sports club ya msimbazi jijini Dar es salaam imeendeleza ushindi wake Mara baada ya kuichapa Mbao fc Magoli Matano bila Majibu katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
Mvua hiyo ya magoli ilianzishwa na mshambuliaji mwenye kasi shiza ramadhani kichuya dakika ya 38 na baadae Emmanueli okwi dakika ya 41 kupitia mkwaju wa penati hivyo kipindi cha kwanza kuisha kwa matokeo ya mbili bila simba ikiongoza
Kipindi cha pili simba waliongeza kasi zaidi ya mashambulizi kulikopelekea Mbao kunyon'gonyea na kuongezwa bao la tatu lililotiwa kimyani na mshambuliaji Emmanuel okwi dakika ya 68 na baadae Erasto Nyoni dakika ya 82 kabla ya mchezaji Gyan kufunga bao la tano dakika ya 86 na kuhitimisha idadi ya magoli Matano kwa sifuri


0 maoni: