Ijumaa, 2 Machi 2018

Fid Q kumtetea Roma BASATA

ad300
Advertisement

Napa fid Q Faridi kubanda ameeleza kutoridhishwa na uamuzi uliotangazwa na naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Magdalena shonza kumfungia kwa miezi sita msanii Roma mkatoliki kufanya Muziki kutokana na wimbo wake wa kibamia kukiuka maadili faridi kubanda amesema

"Ni ukweli sio sahihi kwa sheria kubagua lakini je mnakumbuka kama KIBA100 ilitoka 22 Nov na BasataTanzania mkawaita 7 dec!? Na je mnajua kama miezi 6 haijaisha? "

"Na hili suala la kumfungia msanii  asifanye kazi zake za sanaa kwa miezi sita,kisa tu kwenye mziki wake kuna neno moja au hata 10 yenye  ukakasi sio sahihi...kuzizuia zisichezwe kwenye radio na TV ilikua ni adhabu tosha kabisa BasataTanzania hii tabia ya KUKOMOANA mmeitoa wapi?"

Haya hivyo Fid Q ameomba kukutana na baraza la sanaa ili waweze kutatua suala hilo ili liweze kukaa Sawa na Roma akarejea mwenye kazi ya Muziki

"Kuteleza kupo lakini hiyo hainifanyi mimi nisiwe na imani na nyinyi ndugu zetu @BasataTanzania - naomba tuyajadili haya jumatatu kwenye jukwaa lenu la sanaa"

Nao BASATA kwa upande wao wameeleza kuridhishwa na maombi ya FID Q hivyo kukubaliana kukutana wiki ijayo kujadili suala hilo

Mkuu hili la fursa ya JukwaaLaSanaa tumelimaliza jana. Matarajio yetu mmeshaleta maombi kwa ajili ya suala hili kufanyika wiki ijayo. Karibuni sana.



Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: