![]() |
Advertisement |
Dar es Salaam. Viongozi wakuu wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe wamewasili katika kituo Kikuu cha Polisi kama walivyotakiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wengine ni Katibu Mkuu, Dk Vincent Mashinji, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Viongozi hao wa chama hicho na wengine ambao hawajafika wanaripoti katika kituo hicho ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.
0 maoni: