Ijumaa, 2 Machi 2018

Polisi watano wauwawa nchini Kenya

ad300
Advertisement

Al- Shabaab nchini Somalia
Polisi watano wa Kenya wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya katika shambulio linaloaminika kutekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabaab katika eneo la Fino, katika kaunti ya Mandera kaskazini mwa nchi hiyo.
Naibu kamishena mkuu wa eneo hilo Eric Oronyi, anakisia kuwa kati ya wapiganaji 70 au 100 hivi, waliokuwa na silaha kali, walivamia kambi ya polisi mapema leo alfajiri na kuiteketeza kabisa.
Amesema kuwa maafisa wengine watatu walijeruhiwa, na mmoja wao yuko katika hali mbaya, shirika la habari la Reuters limeongeza.
Al-Shabab "wagawa chakula Somalia"
Al-Shabab washambulia kambi ya jeshi nchini Somali
Kenya yaanza kuangusha mabomu ‘msitu wa al-Shabab’
Bwana Oronyi amesema kwamba washambuliaji hao waliharibu mtambo wa mawasiliano, kabla ya kuvamia kambi hiyo.
"Mnara wa mawasiliano, ambao ulikuwa ukilindwa na polisi wa akiba, ulipigwa bomu na kwa sasa, hakuna mawasiliano yoyote ya simu hata ya rununu katika eneo hilo", amesema Bw Oronyi.
Kundi hilo la wapiganaji, ambalo limekuwa likitekeleza mashambulio mara kwa mara kutokea nchi jirani ya Somalia, mara kwa mara limekuwa likiwalenga maafisa wa usalama na magari ya umma, kuvamia maskani ya watu na matimbo ya mawe na kuwauwa watu wengi kwa kuwapiga

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: