Jumatatu, 29 Oktoba 2018

SAFARI YA MWISHO YA MTANGAZAJI ISACK GAMBA

Mamia ya waombolezaji wamekusanyika katika eneo la hospitali ya jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa mtangazaji  Isaac Gamba aliyefariki dunia Ujerumani.

Ibada ya kumuaga mwandishi wa habari wa idhaa ya Kiswahili DW, Isaac Muyenjwa Gamba, inaendelea Lugalo mjini Dar es Salaam.

Watu mbalimbali, familia, jamaa, ndugu, marafiki ,  Mkuu wa   Idhaa ya kiswahili ya DW pamoja na baadhi ya watumishi wa idhaa, waandishi wa habari wa vyombo vya kimataifa na kitaifa, wasikilizaji na waliokuwa wapendwa wa marehemu wamekusanyika eneo la hsopitali ya  Lugalo kutoa heshima zao za mwisho.

Jumapili, 28 Oktoba 2018

ACT WAZALENDO YAELEZA JINSI SERIKALII ILIVYOVURUGA ZAO LA KOROSHO


Serikali Imevuruga Zao La Korosho, Imeshindwa Kulinda Ustawi na Usalama wa Raia 


A: Utangulizi 


Jana, Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo, ambayo ni Kikao cha Kikatiba ambacho wajumbe wake ni Viongozi wote wa juu wa chama chetu ilikutana katika kikao chake cha kawaida kujadili hali ya chama na hali ya nchi kwa ujumla. 


Pamoja na mambo mengine, pia Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo ilitathmini mwenendo wa  usalama wa nchi na hali ya Uchumi, hususan masuala yanayohusu wakulima na hasa uzalishaji wa zao la Korosho, zao linaloongoza kwa kuingizia nchi yetu Mapato ya Fedha za kigeni kuliko mazao yote kwa ujumla. Hivyo leo, tumewaita hapa kwa niaba ya Kamati ya Uongozi ili kupitia nyinyi tufikishe mawazo, mapendekezo kwa wanaACT Wazalendo pamoja na Watanzania kwa ujumla juu ya masuala hayo mawili.


A: Hali ya Usalama ni Mbaya 


1. Nchi Imejaa Khofu


Wiki ijayo itatimia miaka mitatu ya utawala wa Serikali ya awamu ya Tano, utawala ambao imedhihirika bayana kuwa silaha yake kubwa ya kuendesha nchi ni kwa kuwatia khofu wananchi. Kitu kimoja ambacho utawala huu unaweza kujivunia baada ya miaka mitatu ni khofu kutamalaki kila upande. Maana imegusa mtu mmoja mmoja, imegusa vikundi vya kijamii kama vyama vya siasa (kikiwemo chama tawala), waandishi wa habari, wafanyabiashara, wawekezaji, wakulima, wafanyakazi, asasi za kiraia, wanafunzi, wanasanaa, wavuvi, wanasiasa nk. Kila sehemu nchini kumejaa khofu!


Tanzania katika miaka mitatu ya Rais Magufuli imekuwa ni nchi ya watu kutekwa, kushambuliwa kwa risasi na ‘Watu Wasiojulikana’, kuokotwa miili yao ikiwa imeuawa, kuwekwa kwenye viroba na kutupwa kwenye fukwe za bahari na mito yetu. Ni jambo la kawaida sasa mtu kutekwa au askari kufyatulia risasi makumi na mamia ya wananchi.


Tunayo mifano iliyo wazi, Msaidizi wa Kiongozi wa Upinzani Bungeni, ndugu Ben Saanane, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo na Diwani wa kata ya Kagezi, ndugu Simon Kanguye, na Mwandishi wa Habari za uchunguzi wa gazeti la kila siku la Mwananchi, ndugu Azory Gwanda wamepotezwa, huku watuhumiwa namba moja wakiwa ni vyombo vya dola.


Mpaka sasa hakuna yeyote aliyekamatwa kufuatia tukio la kumpiga risasi nyingi kwa lengo la kumuua Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, ndugu Tundu Lissu, pmaoja na shambulizi kutokea ndani ya eneo la Bunge. Serikali inadhani kwa kuchagua kukaa kimya, damu ya watu hawa itapotea kimyakimya? Haiwezekani!


Miaka hii mitatu tumeshughudia Mamia ya wananchi wenzetu wakiuawa na kupotezwa katika eneo la MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji). Majuzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro, akizungumzia sakata la kutekwa kwa Mohammed Dewji alitoa dondoo kidogo kwamba walilazimika kutumia nguvu kule MKIRU kuwaondosha watu aliodai sasa wamekimbilia Msumbiji. Kwa mara ya kwanza IGP Sirro alikiri kuwa kuna watu wengi waliuwawa. 


ACT Wazalendo Tutafanya Nini?


Chama chetu kimepaza sauti juu ya masuala haya ndani ya miaka hii mitatu, pamoja na Serikali kuamua kutokueleza ukweli au kuchukua hatua kuyazuia, bado hatutakaa kimya. Tutafanya yafuatayo:


• Tutaendelea kusisitiza kuundwa kwa Tume ya Kutafuta Ukweli wa Mauaji ya MKIRU, na kupigania watu wote waliochukuliwa misikitini katika Wilaya za Kilwa na Lindi warejeshwe wakiwa hai ama ndugu na jamaa zao wawlezwe kama wameuawa. 


• Tutaendelea kuhamasisha umma wa watanzania uendelee kushikamana kuwapigania Azory Gwanda, Simon Kanguye na Ben Saanane mpaka pale watakapopatikana au ukweli juu yao kujulikana. Ukweli wa mambo ni kuwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji asingepatikana bila nguvu ya umma. Watanzania wasingepaza sauti naye angepotezwa tu kama Saanane, Kanguye na Azory. 


Watanzania waendeleze mshikamano huu kwa watu wengine ili kukomesha kabisa vitendo hivi vya utekaji na watu kupotea. 


• Tutaendelea kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ijitathmini. Kwa muda mrefu tumepigania mageuzi ya kimfumo na ya kiuendeshaji ndani ya TISS. TISS si usalama wa CCM wala serikali. TISS ni usalama wa taifa. Yanapotea matukio makubwa yanayotishia usalama wa taifa letu, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa anapaswa kuwajibika. TISS ikikaa kimya huku matukio yanayotishia usalama wa wananchi yakikita mizizi, hisia kwamba ‘WATU WASIOJULIKANA ni TISS zitapata uhalali. Wakati umefika kwa Wazalendo ndani ya TISS kuamka na kurejesha hadhi ya chombo hicho.


• Tutaendelea kuyasema bungeni, na katika kila pahala tutakapopata nafasi ya kupaza sauti yetu. Tutafanya hilo la kupaza sauti pamoja na kutambua unyeti wa usalama wa nchi yetu, lakini tukipinga njia ya kuua, kuteka, kupoteza na kutesa wananchi wenzetu kwa kigezo cha kulinda usalama wa nchi, ni njia inayowajaza khofu tu wananchi. Khofu ni ishara ya kukosa uhuru, na bila uhuru watu hawawezi kusemwa kuwa wapo salama. Pia, bila uhuru hakuna maendeleo.


2. Wananchi wengi sana  Wanadaiwa Kuuawa Uvinza 


Wiki iliyopita yalitokea mauaji ya Askari wa jeshi la Polisi katika eneo la mto Malagarasi, kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza, mkoani Kigoma, ambapo Mkuu wa Kituo cha Polisi Nguruka aliuwawa na wanaodaiwa kuwa ni wananchi. Chama chetu kilitoa salaam za rambirambi kwa IGP kufuatia mauaji hayo, kikilaani na kikitaka uchunguzi ufanyika na wahalifu wakamatwe na kufikishwa mahakamani. 


Tumekuwa tukifuatilia kwa kina yote yanayojiri huko Uvinza tangu kuuawa kwa askari Polisi wetu. Tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno, kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa Kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na Polisi, wengine wakisemwa kuuawa hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na jeshi la polisi.


Jeshi la Polisi limekalia kimya suala hili, pamoja na IGP kutembelea eneo hilo la maafa. Haiwezekani kamwe tukio kubwa namna hii kutokea halafu Serikali ibaki kimya bila kutoa maelezo yeyote kwa Wananchi. Uchunguzi wa kina unapaswa kufanywa ili kutambua nini kimetokea pale Mgeta.


ACT Wazalendo Itafanya Nini?


Kwa sasa tunaitaka Serikali ieleze nini hasa kimetokea Mgeta, maelezo hayo yawe ya kina na yawe ya ukweli. Chama chetu kinaendelea kukusanya majina na taarifa za wote wanaodaiwa kuuawa, na kitaweza wazi taarifa husika.


B: Serikali Iwajibike kwa Kuchezea Suala la Korosho 


Kwa wiki mbili sasa mjadala ni juu ya bei ya zao la Korosho. Wakati wa Bunge la Bajeti mjadala ulikuwa mkubwa pia, hasa juu ya hatua ya Serikali kudhulumu fedha za Wakulima wa Korosho zaidi ya shilingi 200 bilioni zilizopaswa kutolewa kwa ajili ya kusaidia uendezwaji wa zao hilo (kurahisisha usambazaji wa pembejeo kama madawa na viatilifu vingine, uendeshaji wa chuo cha Utafiti Naliendele na kujenga mazingira ya kuongeza ubanguaji nchini ili kuongeza thamani ya korosho kwa wakulima wetu na hivyo kuongeza uzalishaji na kipato chao).


Serikali kupitia Bodi ya Korosho huweka bei elekezi ya kuuzwa kwa zao hilo, na kwa mwaka huu bei elekezi ni Shilingi 1,550. Bei hii iliwekwa kwa kigezo kuwa Mkulima alinunua dawa ya Salfa (sulphur) kwa shilingi 32,000 kwa mfuko, hivyo ikikadiriwa kuwa gharama za uzalishaji kwa kila kilo moja ya korosho kwa mkulima ni shilingi 1,350, na hivyo kwa hiyo bei elekezi mkulima anatarajiwa kupata faida ya shilingi 200 kwa kila kilo moja atakayouza.


Ukweli ni Kwamba mwaka 2018 kulikuwa na ulanguzi mkubwa wa Salfa, na mkulima alinunua dawa mpaka shilingi 84,000 kutoka shilingi 14,000 iwapo fedha za Ushuru wa Korosho (exports levy) zingetumika kama ilivyopaswa na Serikali isingezidhulumu. 


Katika minada minne ya TANECU (Tandahimba na Newala), MAMCU (Mtwara, Masasi na Nanyumbu), RUNALI (Ruangwa, Nachingwea na Liwale) na ule wa Lindi Mjini wakulima wamegoma kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya shilingi 2700 (zaidi ya shilingi 1150 kutoka bei elekezi) kwa sababu bei elekezi haikuwa halisi. Zaidi Wakulima wanasema kuwa Serikali iliwaahidi kuwa bei ya kilo moja ya Korosho itafikia shilingi 5,000 kwa mwaka huu kwa sababu kuna wanunuzi kutoka Marekani. 


Maamuzi Mabaya ya Serikali Yatashusha Uzalishaji


Mwaka 2017 Tanzania ilizalisha Korosho tani 331,000 Sawa na ongezeko la 96% ya uzalishaji wa 2016. Kwa uzalishaji huo nchi yetu ilipata fedha za kigeni Dola 542 milioni, Sawa na ongezeko la 100% kutoka Dola 271 milioni za mwaka 2016. Bila Serikali kuingilia mfumo wa Korosho Mwaka 2018 tungepaswa kuzalisha tani 500,000 za Korosho na hivyo ama kuongeza Mapato ya fedha za kigeni au hata kuzuia kuporomoka kwake. 


Bahati mbaya Sana Mwaka 2018 Serikali ikaamua kuwanyanganya Wakulima fedha zao za export levy, shilingi 200 bilioni, na hivyo kuathiri upatikanaji wa Salfa kwa wakulima wa Korosho. Inakadiriwa kwamba uzalishaji unaweza kuporomoka kwa 40%. Habari za ndani zinasema kuwa uzalishaji wa Korosho mwaka 2018 utakuwa chini uzalishaji wa mwaka 2012 ambapo zilishalishwa tani 131,000 tu.


Kutokana na uzalishaji kwenda chini na bei nayo kushuka, wananchi na serikali wote watapungukiwa mapato. Wananchi watapata mapato chini ya shilingi 4,000 kwa kilo waliyouza Mwaka jana na Taifa litapata dola za kimarekani $209m tu kwa bei ya sasa ya soko la dunia ya dola 1.6 kwa kilo. 


Anayepasa kubeba mzigo wa lawama kwenye hili ni Serikali ambayo imekwapua fedha za export levy ambazo zingetumika kwenye utafiti, kununua pembejeo na uendeshaji wa tasnia nzima ya zao la korosho na hivyo kukuza uzalishaji. Kukwapua fedha za export levy ilikuwa ni sawa na mkulima kula mbegu! Tunapotafakari uwezekano wa kushuka kwa uzalishaji uliosababishwa na kukosa pembejeo, tukumbuke kumuwajibisha aliyekula mbegu. 


Udhibiti wa Bei


Uchumi wa nchi nyingi za Kiafrika bado una sifa ya uchumi wa kikoloni ambapo sehemu kubwa ya malighafi yalisafirishwa kwenda nje. Hadi sasa, zaidi ya miaka 60 tangu uhuru wa taifa letu, bado tunasafirisha malighafi ya viwandani kwenda Barani Ulaya, Asia na Amerika. Kwa korosho hali ni hiyohiyo. Kwa msingi huo, kwa sehemu kubwa bei hudhibitiwa na kupangwa nje.


Mwaka 2016/2017 bei ya korosho ilivyopanda tulipoieleza Serikali ya CCM kwamba ongezeko hilo la bei ya korosho hadi kufikia 4000 na zaidi kwa kilo halikutokana na mikakati ya ndani bali hali ya mahitaji ya nje hasa nchini Vietnam tulionekana wazushi na wenye wivu. 


Lengo letu ilikuwa ni kuiamsha serikali ijibidiishe kuimarisha uzalishaji na ubanguaji wa korosho nchini ili kutumia fursa ya bei ya korosho kupanda kuongeza mapato ya serikali na wananchi.  Hakuna aliyetusikiliza. Rais mwenyewe alitamba kwamba amesababisha bei ya korosho kupanda hadi wakulima wa korosho wananywesha mbuzi soda.


Kabla ya msimu wa korosho kuanza, kutokana na ufuatiliaji wetu, tuliijulisha serikali kwamba kuna uwezekano wa bei ya korosho kushuka kiasi kutokana na mwenendo wa soko la dunia. Tuliwataka wajifunze kwa Ivory Coast ambako bei imeshuka kwa zaidi ya nusu. Badala ya kuipokea taarifa hiyo, tuliitwa  wazushi na kwamba bei ya korosho mwaka huu itapanda zaidi kuweza kufikia 5000. Sasa tunaidai bei ya 5000 ambayo serikali iliahidi, inaruka kwamba bei inashuka kutokana na soko la dunia! 


CCM na serikali yake ni mabingwa wa hadaa. Bei ikipanda ni wao wameipandisha. Bei ikishuka, si wao, ni soko la dunia au anatafutwa mchawi kutupiwa lawama kama wanavyofanya sasa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho.


Unawezaje kuwalaumu wafanyabiashara na Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho wakati wewe mwenyewe umeweka bei elekezi ya shilingi 1550 kwa kilo kwa madai ya kwamba mkulima atapata faida ya Tsh. 200 halafu mfanyabiashara ananunua Tsh. 2700 kwa kilo unasema anamnyonya mkulima? Mnyonyaji ni mfanyabiashara au wewe uliyepanga bei elekezi?


Vile vile tuliishauri Serikali kwamba wakati bei ni kubwa sehemu ya fedha za exports levy zitumike kujenga mfumo wa hifadhi ya jamii kwa Wakulima wa Korosho ambapo Wakulima wangepata bima ya afya, kuweka akiba na muhimu zaidi fao la bei (price stabilization) ili kukabili misukosuko ya soko la dunia. Serikali haikutaka kusikia ushauri huu na leo wanahangaika. Ingekuwa wamefanya tulivyoshauri Serikali ingeweza kufidia kushuka kwa bei kwa kuwalipa Wananchi kiasi cha fedha ambacho bei imeshuka ili kuwawezesha kukabili gharama za uzalishaji. 


Tunapendekeza; 


- Serikali inunue Korosho yote kwa wakulima ili kuwalinda na bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya korosho kwenye soko la dunia. Kwa vile malengo ya serikali hayatakuwa kupata faida bali kufidia gharama za manunuzi, bei ya korosho haitashuka sana. Kisha Serikali iwauzie wanunuzi kwa namna wanaona inafaa. Lengo hapa ni kumlinda Mkulima kwa kumpa bei nzuri. 


- Tunarudia tena rai yetu kwa serikali kuanzisha fao la bei kwenye mfumo wetu wa hifadhi ya jamii ili kumlinda mkulima na kushuka kwa bei.


- Tunamtaka Rais Magufuli awaombe radhi Wabunge wa mikoa inayolima korosho kwa kitendo chake cha kuwatisha na kuwadhihaki waliposimama kidete kupigania kutokukwapuliwa kwa fedha za export levy ambazo zingetumika kwenye uendeshaji mzima wa tasnia ya korosho na hivyo kukuza uzalishaji na kuviwezesha chombo ambacho kinasimamia soko la korosho ambacho ni Bodi ya Korosho.


- Tuongeze kasi kwenye ujenzi wa viwanda vya ubanguaji wa korosho ili kuongeza thamani yake badala ya kuendelea kusafirisha korosho ghafi


Mwisho, tunarudia rai yetu ya mara zote kuwa kuongoza ni maarifa, si mabavu. Serikali iwe tayari kupokea mawazo chanya kwa ustawi wa taifa letu. Tanzania ni yetu sote


Kabwe Z. Ruyagwa Zitto 

Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo

Oktoba 28, 2018

Dar es Salaam

Zitto: TISS SIO USALAMA WA CCM WALA SERIKALI

Chama cha ACT wazalendo kimesema kuwa kitaendelea kuitaka Idara ya usalama wa Taifa (TISS) Kujitathimini na kwamba mageuzi yanahitajika katika utendaji kazi wa chombo hicho na kurejesha hadhi ya chombo hicho

akizungumza na wanahabari hii leo kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema kuwa

"TISS si usalama wa CCM wala serikali.Yanapotokea matukio makubwa yanayotishia usalama wa taifa letu,Mkurugenzi anapaswa kuwajibika"

Pia akigusia suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji Zitto kabwe amesema kuwa baada ya kupatikana kwa Mohammed Dewji kama taifa bado lina jukumu kubwa la kuhakikisha hao ambao hawajapatikana wanapatikana wakiwa hai au kama hawako hai ndugu zao wapewe nafasi ya kuifanya dua na sala.

Katika hatua nyingine chama cha ACT wazalendo kimeitaka serikalii iwajibike katika sakata la korosho na kusema kuwa kulikua na ulanguzi mkubwa wa salfa ,na mkulima alinunua dawa shilingi 84,000 kutoka shilingi 14,000 iwapo fedha za Ushuru wa Korosho (exports levy) zingetumika kama ilivyopaswa na Serikali isingezidhulumu."

Lakini pia chama hicho kimeishauri serikalii kuongeza kasi ya ujenzi wa viwanda vya kubangua korosho nchini ili kuongeza thamani ya korosho yake badala ya kuendelea kusafirisha korosho ghafi

Vile vile chama hicho kimeitaka serikalii kununua korosho za wakulima kwa bri ya mwaka jana ya shillingi 4000 ili yenyewe(serikalii) iwauzie wenye minada ili kuepusha hasara kwa mkulima

Pia Chama cha ACT kimemtaka Rais aombe radhi kwa wabunge waliokuwa wakitetea zao la Korosho kutokana na kauli yake ya kuwatisha kiasi cha kusema angeanza kwa kupiga mashangazi zao. Zitto Kabwe amesema kuwa

"Tunamtaka Rais Magufuli awaombe radhi wabunge wa kusini ambao aliwadhihaki wakati wanapigania fedha za export levy ambazo zingesaidia kuinua zao la korosho nchini, kuomba radhi ni uungwana"


Lakini pia Zitto Kabwe ameitaka serikali kuongoza nchi kwa maarifa na si kwa mabavu
"Tunarudia Rai yetu ya mara zote kuwa kuongoza ni maarifa, si mabavu. Serikali iwe tayari kupokea mawazo chanya kwa ustawi wa taifa letu. Tanzania ni yetu sote"

Katika hatua nyingine chama cha Act wazalendo kimetangaza kutoshiriki katika chaguzi za marudio kutokana na kutoridhishwa na hali ya kisiasa hapa nchini.


Ijumaa, 12 Oktoba 2018

LOWASSA NCHI IMEJAA HOFU NA CHUKI

Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowassa amesema nchi haina viashiria vya uvunjifu wa amani katika chaguzi za marudio bali wananchi wamejengewa hofu na chuki wawachague watu wasiotaka.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 12, 2018  wakati akichangia mjadala katika mdahalo wa kumbukizi ya miaka 19 ya Tanzania bila Mwalimu Julius Nyerere .

“Mzee Butiku (Joseph- mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere) amesema jana (katika mdahalo huo) walizungumza juu ya  amani na wakasema kuna viashiria vya kukosekana kwa amani. Mimi neno hilo halinitoshi,  msamiati huo nauhitaji uwe mkali kidogo,” amesema Lowassa.

“Mimi naona nchini kuna hofu na chuki. Inajengwa hofu kubwa kwa wananchi inayowafanya wawachague watu wasiotaka kuwachagua.”

Lowassa ametoa mfano wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Monduli, akibainisha kuwa  kulikuwa na gari za vyombo vya ulinzi na usalama  45, pamoja na magari ya maji ya kuwasha.

“Kamji kale (Monduli) kakawa kamezungukwa na magari ya jeshi utafikiri kuna vita. Vitu hivyo vinafanywa kwa kutumia vyombo vya dola kusimamia uchaguzi, inakuwa ni taabu sana,” amesema.

Amesema wenzake waliouponda Uchaguzi Mkuu wa Kenya,  binafsi aliupenda kwa sababu waliwafuata watu waliofanya makosa kwenye tume ya uchaguzi kwa kuwapeleka mahakamani na kuadhibiwa.

Amesema nchini inapaswa watizamwe watu hao kwa sababu wanaosimamia uchaguzi Tanzania ni watumishi wa Serikali na wanalipwa na Serikali, hivyo hawawezi kuacha Serikali ianguke.

Amesema miongoni mwa watumishi hao, wapo waliosema waziwazi kuwa hawawezi kuiacha Serikali ianguke, kufafanua kuwa zimewekwa mbinu ili wapinzani wasishinde chaguzi za marudio.

“Kuna chuki mbaya sana  imefikia hatua mwanachama wa Chadema na CCM wanachukiana. Inatia hofu kwa wananchi,” amesema.

Amesema ipo haja ya kuzungumza na wananchi  ili waachane na chuki  na kutokuwa na hofu huku akigusia mapendekezo ya Katiba Mpya yaliyotolewa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.

“Haitoshi kuwaambia kuna viashiria (vya hofu na chuki), waambiwe wazi hili na hili si sawa, ”amesema Lowassa.

Amesisitiza kuwa bila demokrasia hakuna haki na  bila haki hakuna demokrasia.

Alipoanza kuchangia mjadala huo, mbunge huyo wa zamani wa Monduli, alianza kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akisema kuwa ameusikia moto alioanza nao.

LOWASSA WANANCHI WAMEJENGEWA HOFU NA CHUKI

Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowassa amesema nchi haina viashiria vya uvunjifu wa amani katika chaguzi za marudio bali wananchi wamejengewa hofu na chuki wawachague watu wasiotaka.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 12, 2018  wakati akichangia mjadala katika mdahalo wa kumbukizi ya miaka 19 ya Tanzania bila Mwalimu Julius Nyerere .

“Mzee Butiku (Joseph- mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere) amesema jana (katika mdahalo huo) walizungumza juu ya  amani na wakasema kuna viashiria vya kukosekana kwa amani. Mimi neno hilo halinitoshi,  msamiati huo nauhitaji uwe mkali kidogo,” amesema Lowassa.

“Mimi naona nchini kuna hofu na chuki. Inajengwa hofu kubwa kwa wananchi inayowafanya wawachague watu wasiotaka kuwachagua.”


Lowassa ametoa mfano wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Monduli, akibainisha kuwa  kulikuwa na gari za vyombo vya ulinzi na usalama  45, pamoja na magari ya maji ya kuwasha.

“Kamji kale (Monduli) kakawa kamezungukwa na magari ya jeshi utafikiri kuna vita. Vitu hivyo vinafanywa kwa kutumia vyombo vya dola kusimamia uchaguzi, inakuwa ni taabu sana,” amesema.

Amesema wenzake waliouponda Uchaguzi Mkuu wa Kenya,  binafsi aliupenda kwa sababu waliwafuata watu waliofanya makosa kwenye tume ya uchaguzi kwa kuwapeleka mahakamani na kuadhibiwa.

Amesema nchini inapaswa watizamwe watu hao kwa sababu wanaosimamia uchaguzi Tanzania ni watumishi wa Serikali na wanalipwa na Serikali, hivyo hawawezi kuacha Serikali ianguke.

Amesema miongoni mwa watumishi hao, wapo waliosema waziwazi kuwa hawawezi kuiacha Serikali ianguke, kufafanua kuwa zimewekwa mbinu ili wapinzani wasishinde chaguzi za marudio.

“Kuna chuki mbaya sana  imefikia hatua mwanachama wa Chadema na CCM wanachukiana. Inatia hofu kwa wananchi,” amesema.

Amesema ipo haja ya kuzungumza na wananchi  ili waachane na chuki  na kutokuwa na hofu huku akigusia mapendekezo ya Katiba Mpya yaliyotolewa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.

“Haitoshi kuwaambia kuna viashiria (vya hofu na chuki), waambiwe wazi hili na hili si sawa, ”amesema Lowassa.

Amesisitiza kuwa bila demokrasia hakuna haki na  bila haki hakuna demokrasia.

Alipoanza kuchangia mjadala huo, mbunge huyo wa zamani wa Monduli, alianza kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally akisema kuwa ameusikia moto alioanza nao.

Alhamisi, 11 Oktoba 2018

JE MO DEWJI NI NANI..?

JE MO DEWJI NI NANI..?

Mo alizaliwa tarehe 8 Mei mwaka 1975, ikiwa na maana kwamba kwa sasa ana miaka 43.

Alizaliwa eneo la Ipembe, Singida maeneo ya katikati mwa Tanzania.

Kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes, ana utajiri wa dola bilioni 1.5

Ni wa pili miongoni mwa watoto sita wa Gulamabbas Dewji na Zubeda Dewji.

Alisomea elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Arusha na baadaye akasomea elimu ya sekondari katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.

Alihamishiwa Marekani kwa masomo zaidi ya sekondari katika jimbo la Florida mwaka 1992.

Alisomea chuo kikuu cha Gerogetown jijini Washington DC na kuhitimu mwaka 1998 akiwa na shahada ya kwanza katika biashara ya kimataifa na fedha, na masuala pia ya dini. Miongoni mwa watu mashuhuri waliosomea chuo kikuu hicho ni rais Bill Clinton, rais wa zamani wa Ufilipino Gloria Arroyo, Mfalme wa Jordan Abdullah na wachezaji wa NBA kama vile Allen Iverson na Patrick Ewing.

Baada ya kufuzu, alirejea Tanzania na kuanza kushiriki katika usimamizi wa kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970.

Fedha
Image captionFedha

Alihudumu kwa miaka miwili kabla ya kuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, wadhifa ambao ameendelea kuushikilia hadi sasa.

Mo ndiye tajiri namba moja Afrika Mashariki, na pia miongoni mwa matajiri wa umri mdogo zaidi Afrika.

Kampuni ya METL, kwa mujibu wa Forbes, ilifanikiwa kwa kununua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa.

METL ina viwanda vya kutengeneza nguo na  bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.

Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.

Kwa mujibu wa tovuti yake, METL inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.

Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

METL ina shughuli zake katika nyingi barani Afrika na ina malengo ya kujipanua zaidi katika maeneo zaidi.

Inaendesha shughuli zake Tanzania, Uganda, Sudan Kusini, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Malawi, Msumbiji na Zambia, ambapo huajiri watu zaidi ya 28,000.

Image copyrightAFPMo Dewji

Shughuli za MeTL huchagia 3.5% ya jumla ya pato la taifa (GDP) la Tanzania.

Kiwango cha wastani cha ukuaji wa mapato ya kampuni hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2014 kutoka $30 milioni hadi $1.3 bilioni kilikuwa ni 200%.

Lengo la kampuni hiyo ni kuongeza mapato ya taifa lake hadi $5bn kufikia mwaka 2020, pamoja na kuwaajiri watu 100,000.

Mo Dewji ameorodheshwa wa 17 kwenye orodha ya mabilionea barani Afrika na wa 1561 duniani kwenye orodha ya mabilionea mwaka 2018.

Wakati mmoja kampuni yake ilianzisha Mo Cola kushindana na Coca Cola.


Dewji ni Mtanzania pekee aliyesaini mkataba mwaka 2016 wa kutoa kwa wahitaji nusu ya mali yake.

Mo Dewji Foundation ndio asasi ambayo aliianzisha mwaka 2014 ili kutekeleza nia yake hiyo na kazi yake kubwa ni kusaidia watanzania wasiojiweza kwa upande wa afya, elimu na maendeleo jamii.

Mbali na biashara na shughuli za jamii Mo Dewji amewahi kuwa mwanasiasa na mwaka 2005 mpaka 2015, Mohamed Dewji alikuwa mbunge wa Singida Mjini.

Alijiingiza katika siasa mara ya kwanza mwaka 2000 ambapo alishinda uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo hilo, wakati huo akiwa na miaka 25, lakini akazuiwa kuwania kwa madai kwamba alikuwa bado mdogo wa umri.

Alistaafu kutoka kwenye siasa baada ya kuhudumu mihula miwili.

Mwaka 2012, alitawazwa Kiongozi Mdogo Duniani kwa Kiingereza Young Global Leader (YGL) wakati wa kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa uchumi Duniani (WEF).

Mwaka 2015, alitajwa kuwa bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika na jarida la Forbes na baadaye akatawazwa Mtu Mashuhuri wa Mwaka wa Forbes.

Mwaka uliopita, alishinda tuzo ya Afisa Mkuu Mtendaji bora wa Mwaka Afrika katika mkutano mkuu wa maafisa wakuu watendaji wa Afrika.


Mke wa Dewji huitwa Saira, aliyekuwa wanapendana tangu utotoni, na wamejaliwa watoto watatu Nyla, Abbas na Mahdi. Alifunga ndoa mwaka 2001. Mo na mke wake walikutana Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam.


Dewji pia ni mpenzi wa michezo na amewekeza katika klabu ya mpira ya Simba inayocheza katika Ligi Kuu ya Tanzania ambapo ni mfadhili mkuu kwa sasa.

Amekuwa akifadhili ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Jumanne, 9 Oktoba 2018

Mwalim Nyerere died in London

The former president of Tanzania, Dr Julius Nyerere, one of Africa's most charismatic postcolonial leaders, died in a London hospital yesterday, aged 77.

"Dear Tanzanians, it is with great shock and sorrow that I announce our beloved father of the nation, Julius Kambarage Nyer ere, is dead," President Benjamin Mkapa said in a national television and radio address in Dar-esSalaam.

Dr Nyerere was one of the leading figures in Africa's struggle for independence and in its post-colonial era. He led his country to independence from Britain in 1961 and served as president from 1962 to 1985, when he became one of the first post-colonial African leaders to leave office voluntarily.

Chronic leukaemia was diagnosed last year, and he was admitted to St Thomas's Hospital last month. On October 1st he went into intensive care and suffered a major stroke last week.

"He died at 10.30 a.m. Tanzanian time [8.30 Irish time] at St Thomas's Hospital in London where he was admitted to undergo treatment for leukaemia on September 24th," Mr Mkapa said.

Tanzanian state radio played funeral music while its television station ran file video of Dr Nyerere.

His wife, Maria, and six of his eight children had been at his bedside in recent days, as well as his former vice-president, Mr Rashid Kawawa.

Although economic disaster, due partly to a Ugandan invasion by Idi Amin, falling commodity prices and corruption, left Tanzania as one of Africa's poorest nations, Dr Nyerere's tenure brought major advances in health and education. He governed with an authoritarian hand but was widely admired for his integrity and intellect.

In Tanzania and across much of Africa, Dr Nyerere is best known as Mwalimu, the Kiswahili word for "teacher".

"I know the death of the father of the nation is going to shock and dismay all Tanzanians," Mr Mkapa said. "Others will be filled with great doubt and fear. Mwalimu built a foundation of unity in our country and he fought for the freedom of all. I assure all Tanzanians Mwalimu left a firm foundation," Mr Mkapa said.


fter his retirement as president, he remained one of Africa's most respected elder statesmen, playing an important advisory role in Tanzanian and regional politics. His last mission was to mediate talks aimed at ending a six-year civil war in neighbouring Burundi.

Dr Nyerere last visited Ireland in November 1996, when he spoke at a a seminar in Dublin organised by Concern and Oxfam.

An obituary will be published in tomorrow's paper