![]() |
Advertisement |
Kamati ya Bunge la Uingereza limemtaka Mkurugenzi wa Facebook, Mark Zuckerberg afike mbele yake ili kujibu maswali kuhusu utumiaji usio halali wa taarifa kutoka katika mtandao wake katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2016.
Kampuni ya Uingereza iitwayo Cambridge Analytica inatuhumiwa kutumia taarifa toka zaidi ya akaunti milioni 50 za Facebook kumsaidia Trump kupata ushindi mwaka 2016 ingawa inakataa tuhuma hizo.
Wakati hayo yakitokea, Bodi ya Kampuni ya uvunaji data ya Cambridge Analytica ambayo inatuhumiwa katika sakata hili, imemsimamisha kazi Mkurugenzi wake ili kupisha uchunguzi.
0 maoni: