Jumatatu, 14 Mei 2018

Marekani kufungua ofisi za ubalozi Mjini Jerusalem

ad300
Advertisement


Marekani itafunguq ubalozi wake mpya mjini Jerusalem hatua ambayo imesifiwa na Israel na kulaaniwa na Wapalestina ambao wanakusanyika kwa maandamano makubwa.






Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.

Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.

Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina amboa wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mkuu.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inahutaja mji huo kuwa wake na usiogawanwa

Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.


Ubalozi wa mdogo utaanza kutoa huduma kuanzia leo Jumatatua kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.

Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.

Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 kuanzishwa taifa la Isreal.

Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale amboa watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.

Image copyrightREUTERSIvanka Trump greets US Ambassador to Israel David Friedman (L) with her husband Jared Kushner (R) at Ben Gurion International Airport, near Tel Aviv
Image captionIvanka Trump akimsalimia balozi wa Marekani nchini Israel David Friedman pamoja na mumewe Jared Kushner (kulia) baada ya kuwasili Israel

Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalzo huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo

Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.

Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.

Israel na Palestina wanafanya nini?

Image copyrightGETTY IMAGESAn Israeli man wearing US flag at a march in Jerusalem. Photo: 13 May 2018
Image captionIsrael imekuwa ikisherehekea

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa wito kwa nchi zote kujiunga na Marekani na kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameutaja uamuzi wa Trump kama dafrao ya karne.

Image copyrightEPAPalestinians in the West Bank protest against the opening of the US embassy in Jerusalem. Photo: 13 May 2018
Image captionWapalestina wameandamana kupinga kuhamishwa kwa ubalozi wa Marekani

Maefu ya Wapalestina wanakusanyika kuandamana kwenye ua unaotenganisha Israwl na ukanda wa Gaza.

Muda wa kuhamishwa ubalozi huo umezua wasi wasi wa kongezeka msukosko huko Gaza

@source BBC

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: