![]() |
| Advertisement |
Msanii wa kizazi kipya Afrika Nasseb Abdul maarufu kama diamond platinums Jana jumatatu amekabidhiwa rasmi leseni ya kuendesha matangazo ya vyombo vya habari anavyovisimamia wasafi FM na wasafi televisheni akieleza hilo katika ukurasa wake wa Instagram diamond amesema kuwa
"Leo tulikabidhiwa Rasmi Leseni ya wasafitv na wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni , Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma...Shukran Nyingi ziifikie Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamuhuri nzima ya Muungano wa Tanzania... Ma raisi wetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison Mwakiyembe."
Lakini pia diamond amesema kuwa lengo la kuanzisha vyombo hivi ni kutengeneza ajira kwa wanahabari na watu wenye uwezo na taaluma ya utangazaji
"Tamanio letu ni kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji ambao pengine hawajapata nafasi bado....kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi tusingekuwepo....lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni"
Ikumbukwe kuwa Diamond platnumz wiki hii yupo Zanzibar kwenye mashindano ya kutafuta vipaji vya utangazaji maarufu kama wasafi presenters search yatakayoanza kurindima siku ya jumanne
Diamond platnumz anakuwa Msanii wa kwanza kumiliki vyombo vya habari kwa maana ya radio na television nchini Tanzania


0 maoni: