![]() |
| Advertisement |
Msanii aliyetamba kwa kibao chake cha "Amina" Sanaipei Tande ameeleza Mashabiki wake kuwa kwa sasa hana nyimbo yoyote ya kushirikishwa na nyimbo nyingi alizoziandika ni za binafsi na amesema kuwa kolabo zitakuja baadae
"So kwa saivi Niko pale ambapo najaribu kuchagua direction yangu lakini definitely baada ya Amina kina project nyingi sana ambazo ni meziandika na wala si makolabo kolabo ziko kando ni vitu ambazo zitakuja baadae"
Aidha msanii huyo ameeleza kuwa anauwezo wa kufanya mziki wa aina tofauti tofauti ila kwa sasa anatafuta mwelekeo
"Na si kwamba eti mi sina direction lakini Mimi ni msanii nayeweza kuimba nyimbo za aina yoyote au I can think out of the box...I can see out of the box ila nataka kujiweka niwe na direction niwe na Identity yangu kama sanaipei ukimsikiliza ni nyimbo aina gani anazo imba"
Vile vile Msanii huyo amewashukuru Mashabiki zake wa Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla kwa kupokea kazi zake na ameahidi kufanya kazi kwa bidii
Source: kingsfm


0 maoni: