![]() |
| Advertisement |
Mbunge wa kigoma mjini kupitia chama cha ACT wazalendo zitto zuberi kabwe amejiuliza Maswali na kutoa majibu yake kupitia mtandao wake wa facebook zitto ameandika
Wakulima wanalalamika kuhusu pembejeo na masoko ya mazao yao. Wafugaji wanalalamika Kuhusu mifugo yao kuuliwa na bei kuporomoka. Wavuvi wanalalamika nyavu zao kuchomwa na kuzuiwa kuuza mazao yao ya samaki. Wafanyabiashara wanalalamika Biashara kuanguka na mabenki kutowapa mikopo. Wafanyakazi wa Umma wanalalamika kufungwa hovyo na Wakuu wa Wilaya na kufukuzwa kazi bila kufuata sheria. Wafanyakazi wote wanalalamika makato makubwa kwenye mishahara yao. Vijana wanalalamika kukosa ajira licha ya kusoma na kumaliza hata stashahada na shahada na shahada za uzamili. Wafanyabiashara wadogo wanalalamika hawana mitaji. Watoto wa kike wanazuiwa kuendelea na masomo wakipata uja uzito. Wanasiasa wa Upinzani wanalalamika kuzuiwa kufanya shughuli za siasa bila bugudha za vyombo vya dola. Wananchi wanalalamika kunyimwa Uhuru wa kujieleza. Vyombo vya Habari vinalalamika kunyimwa Uhuru wa Habari na kuingiliwa Uhuru wa uhariri ( editorial independence) kiasi cha baadhi ya wahariri kusimamishwa kazi na waajiri wao.
Nani halalamiki? Jeshi? Polisi? Usalama? Wabunge? Wanachama wa Chama tawala?
Lakini pia kiongozi huyo wa upinzani alisisitiza juu ya msimamo wake wa kuhitaji kuwepo na mkutano wa kitaifa kujadili hali iliyopo hivi sasa
Nani halalamiki? Tukae tujadiliane kama Taifa. Mkutano Mkuu wa Hali ya Nchi ( State of The Nation Conference - A Sovereign Conference ) ufanyike, with or without ridhaa ya Watawala.
Organize. Don’t Agonize - Kwame Nkrumah


0 maoni: