![]() |
Advertisement |
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameshtakiwa kwa rushwa iliyohusishwa na mkataba wa silaha za miaka ya 1990.
Kesi hiyo iliyosomwa Leo katika mahakama kuu nchini Afrika kusini hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa na kurejewa tena mpaka Juni 8.
Jacob zuma Anakabiliwa na mashtaka 16 ya rushwa, ikiwepo udanganyifu na utakatishaji wa fedha,
Mr Zuma, ambaye alijihudhuru nafasi ya uraisi mwezi Februari, amekataa makosa yote.
Wafuasi wake walishuka kwenye jiji hilo kwa mkutano wake, wakati wakosoaji wake wanafikiria hatua ya mahakama ni ya muda mrefu
Mr Zuma na timu yake ya kisheria wanasisitiza mashtaka hayo yanatokana na kisiasa.
0 maoni: