![]() |
Advertisement |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amemwambia Rais John Magufuli kuwa wachimbaji wadogo wameanza kulipa kodi miezi mitatu iliyopita.
Akifanya utambulisho wa wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite mbele ya Rais, leo Aprili 6, Mnyeti amesema kwa muda mrefu wachimbaji wadogo hawakuwa na mazoea ya kulipa kodi.
“Lakini baada ya kupewa mahesabu yao na Mamlaka ya mapato(TRA) wameanza kulipa kodi miezi mitatu iliyopita,” amesema
Amesema wale wenye mabavu watakaokaidi kulipa kodi, watashughulikiwa na ngazi ya mkoa.
"Tunakupongeza sana kwa hatua hii ya ujenzi huu wa ukuta kwa niaba ya wananchi wa Manyara, " amesema Mnyeti.
0 maoni: