![]() |
Advertisement |
Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, George Mkuchika imeagiza kurejeshwa kazini watumishi wa umma 1370 waliokuwa na elimu ya Darasa la saba wakaachishwa kazi na kuagiza walipwe mishahara yao yote ya kipindi ambacho hawakuwepo kaziniakizungumza bungeni mjini Dodoma hii Leo waziri Mkuchika amesema
"Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu, za mikataba au za muda ambao walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa utumishi wa mwaka 2004, warejeshwe kazini mara moja." -Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais,Utumishi George Mkuchika.
"Watumishi hao walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa umri kila mmoja."
Uamuzi huo umekuja kutokana na mbunge wa geita Joseph kasheku maarufu kama "Msukuma"kuitaka serikali kuwarudisha wafanyakazi hao kazini akizungumza bungeni mjini Dodoma mbunge huyo alipendekeza kuwa wabunge waiiombe serikali kuwarejesha watumishi hao kazini badala ya kuwalipa fidia na kuenda mbali zaidi kwa kuitaka serikali kuwafukuza wabunge walioishia darasa la saba bungeni kama watashindwa kuwarudisha wafanya kazi hao kazini
0 maoni: