![]() |
Advertisement |
Mamia ya wanawake waliotelekezwa baada ya kuzalishwa na waume zao wamejazana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyetangaza kuanza kuwasikiliza.
Kumekuwa na mafuriko ya wanawake wanaoingia kwa kusukumana kwenye ofisi hizo hali iliyowalazimu walinzi kufunga geti ili walio ndani wahudumiwe.
Wanasheria na wafanyakazi wengine wa ofisi hiyo wanaendelea kuwasikiliza wanawake hao wengi wao wakiwa wamebeba watoto wao.
Wakizungumza na MCL Digital leo, Aprili 9 wanawake hao wamesema wingi wao unaweza kusababisha baadhi yao kushindwa kusikilizwa.
"Nilitelekezwa na watoto wanne kwenye nyumba ya kupanga, nimekuwa kama ombaomba nashukuru Makonda ameona kilio chetu lakini kwa umati huu naogopa sana,"amesema mwanamke mmoja.
Wapo waliolala kwenye ofisi hizo huku wengine wakianza kuwasili tangu saa tisa za usiku.
Vimetengwa vyumba maalum zikiwamo kumbi zilizo katika ofisi hizo kwa ajili ya kusikiliza kilichowasibu wanawake hao. wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ameanza kusikiliza malalamiko kutoka kwa wanawake waliozalishwa kisha kutelekezwa na wanaume.
Shughuli hiyo ambayo itadumu kwa siku tano, inafanyika katika ofisi za mkuu huyo wa mkoa, Ilala Boma, huku idadi kubwa ya wanawake na watoto ikijitokeza.
Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa kutokana na utaratibu huo, hofu imetanda kwa baadhi ya viongozi wa serikali, dini, wanasiasa na maofisa waliowapa mimba kisha kuwatelekeza wanawake.
Pia, imedaiwa kuwa hali ni mbaya kwa wanaume viwembe, hususani waliochepuka nje ya ndoa zao, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawataki kujulikana kama wamezaa nje ya ndoa ili kuficha fedheha.
Wengine ambao mambo yao yatawekwa hadharani ni vigogo waliowazalisha wasaidizi wa kazi za ndani pamoja na wafanyakazi wao maofisini.
Akizungumza wakati wa kutangaza operesheni hiyo, makonda alisema amebaini baadhi ya viongozi serikalini, wabunge, vionozi wa dini na viongozi wa vyama vya siasa, wanahusika kwa kiasi kikubwa kuwazalisha wanawake na kuwatelekeza.
“Wengi waliowapa mimba wanawake ni watu wenye ndoa, hivyo hawataki watoto au wanawake hao wajulikane ili kulinda ndoa zao. Vigezo vyao ni kutomtambua mtoto wa nje,” alisema.
Aliisema katika kuficha haki ya watoto, baadhi ya viongozi wameamua kuanzisha vituo vya watoto yatima ambapo ndani ya vituo hivyo huwahifadhi watoto waliozaliwa nje ya ndoa.
“Je, ni halali kwa mtoto mwenye baba na mama, tena wenye kipato cha kutosha kuhifadhiwa katika vituo vya yatima?” alihoji makonda.
Aliongeza “Tunao viongozi wengi wa serikali waliotelekeza kinamama na mtawashuhudia hapa.”
Alisema kwa mwanaume ambaye atakataa mtoto, ataingizwa kwenye gari na kupelekwa kwenye ofisi ya mkemia mkuu kwa ajili ya kupimwa vinasaba (DNA).
“Hadi tumjue mtoto ni wa nani, hivyo na nyie kinamama muwe wakweli, siyo kusingizia wanaume. Ukija hapa uwe na uhakika na mwanaume husika,” alisema.
0 maoni: