![]() |
| Advertisement |
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha katika ukurasa wake was Twitter kwamba Urusi inafaa 'kujiandaa' kwa kombora litakalorushwa nchini Syria.
Maafisa wakuu wa Urusi walitishia kujibu shambulio lolote la Marekani. Bwana Trump aliahidi kujibu vikali madai hayo ya shambulio la kemikali.
Serikali ya Bashar al-Assad ambayo hupokea usaidizi wa kijeshi kutoka Urusi imekana kuhusika na shambulio hilo la kemikali.
Katika chapisho lake la Twitter, bwana Trump alimuita rais Assad 'mnyama anayetumia gesi kuua watu'.
Siku ya Jumamosi, wanaharakati wa Syria, waokoaji na maafisa wa matibabu walisema kuwa mji huo wa Douma unaodhibitiwa na waasi katika jimbo la mashariki la Ghouta ulishambuliwa na vikosi vya serikali kwa kutumia mabomu yalio na sumu.
Shirika la matibabu linaloshirikisha mataifa ya Syria na Marekani limesema kuwa watu 500 walipatikana na dalili za kushambuliwa na kemikali.

Image captionRais Vladmir Putin wa Urusi
Siku ya Jumatano, shirika la afya duniani WHO lilitaka kuingia katika eneo hilo ili kuthibitisha ripoti kutoka kwa washirika wake kwamba watu 70 walifariki, ikiwemo 43 waliokuwa na ishara za kushambuliwa na kemikali za sumu.
Marekani na washirika wake Ufaransa na Uingereza wamekubali kufanya kazi pamoja na wanaaminika kujiandaa kutekeleza shambulio la kijeshi.
Je Urusi inasema nini?
Serikali ya Urusi imetaja ripoti za shambulio la kemikali kama uchokozi unaolenga kuthibitisha haki ya Ulaya kumuingilia mshirika wake, Syria.
Maafisa kadhaa wa Urusi wameonya kuhusu jibu la Urusi iwapo Marekani itashambulia huku Alexander Zasypkin , ambaye ni balozi wa Urusi nchini Lebanon akiregelea onyo la kiongozi wa jeshi kwamba makombora yatatunguliwa huku maeneo yanayotoka yakilengwa.


0 maoni: