![]() |
Advertisement |
Wanasheria kutoka Chama cha Wanasheria wa Tanganyika(TLS) kwa umoja wao leo wamemchagua wakili Fatma Karume kuwa Rais mpya atakayekiongoza chama hicho.
Fatma Karume anachukua nafasi ya Mwanasheria mwenzake Tundu Lisu ambaye amemaliza muda wake.
Hii ni baada ya kuwagaragaza wagombea wenzie watatu ambao ni, Simba Ngwilimi, Musa Mwapongo na Godfrey Wasonga.
Wakati kwa upande wa Zanzibar wanasheria wa Nzanzibar wamemchagua
Wakili Omar Said Shaaban kuwa Rais Mpya wa chama cha Wanasheria Zanzibar(ZLS).
Awali Rais wa TLS anayemaliza muda wake TunduLissu aliwatakia kira raheri Mawakili katika uchaguzi wa leo, kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuendesha taasisi hiyo kwa uhuru bila kuingiliwa.
Huku akiwataka mawakili hao kuwakataa wagombea watakaoathiri uhuru wa TLS kwa kushirikiana na maadui wa Utawala wa Sheria.
Katika uongozi wake Lissu amefanikiwa kutekeleza mambo makubwa matatu;
1) Kuanzisha mchakato wa Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya TLS.
2) Kupunguza ada za Mawakili.
3) Kufumua mfumo wa usimamizi wa fedha wa taasisi hiyo ambayo ilikuwa ikituhumiwa kwa matumizi mabaya.
Ushindi huu unamfanya Fatma kuingia kwenye historia ya kuwa mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo toka kuanzishwa kwa chama hicho cha mawakili zaidi ya miaka 60 iliyopita. Rais wa kwanza wa TLS mwanamke ni Judge Joaquine De Melo
0 maoni: