![]() |
Advertisement |
Timu ya singida united ya mkoani singida inayocheza ligi kuu soka Tanzania bara imekanusha kufungiwa kwa mchezaji wake Daniel Lyanga
Taarifa zilizoelezwa ni kuwa mchezaji Daniel Lyanga wa singida united amefungiwa na shirikisho la soka Duniani FIFA kutokana kusajiriwa katika Timu ya singida United ilihali akiwa bado na Mkataba na timu yake ya zamani ya Fanja Fc Ya nchini Oman
Taarifa kutoka singida united zinasema kuwa mchezaji huyo hajafungiwa kwa miezi sita kama inavyoeleza Bali ITC yake ilichelewa kutokana na mda wa usajili kuisha kabla ya kuikamilisha
Mchezaji wetu Daniel Lyanga hajafungiwa miezi sita usajili wake ulihusisha timu zote mbili singida united na fanja Fc ikiwepo malipo ya gharama za mkataba aliokuwa nao Kule Fanja Fc
Kilichokuwepo ni kwamba ITC yake ilichelewa kutokana na dirisha dogo la usajili kufungwa sisi na TFF tuliandikiwa barua na FIFA kwamba ITC ya Lyanga itakamilika mbaka pale dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa mwezi July 2018
0 maoni: