Alhamisi, 1 Machi 2018

Roma Afungiwa Miezi Sita kutojihusisha na muziki

ad300
Advertisement

Msanii Roma Mkatoliki afungiwa miezi sita kutojihusisha na sanaa ya muziki kutokana na kutotii agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lililomtaka kubadilisha maudhui ya wimbo wake wa kibamia Msanii wa Bongo Fleva, Roma Mkatoliki amefungiwa miezi sita kutojihusisha na Muziki ikiwa ni kutekeleza azma ya Serikali kwa kile kinachodaiwa kukiuka maadili ya jamii za kitanzania kwenye wimbo wake wa "KIBAMIA".

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, amesema kuwa Roma amedharau wito wa serikali ambapo leo aliitwa ili ahojiwe   kutokana na wimbo wake huo ikiwa ni hatua ya pili mara baada ya Baraza la Sanaa Nchini Basata kumuita na kumtaka arekebishe baadhi ya sehemu katika wimbo huo.

"Tumempigia simu mara kadhaa hajapokea, tumemtumia meseji anasoma lakini hajibu chochote hivyo hiyo ni dharau na hatuendelei kudili na mtu mmoja wasanii ni wengi ambao wanahitaji msaada kutoka kwetu" alisema Shonza.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: