Jumatatu, 5 Machi 2018

Kashfa Nzito waamuzi Tanzania

ad300
Advertisement

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF linaendelea na uchunguzi juu ya tuhuma za kupanga matokeo (Match fixing) zinazowakabili waamuzi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa ya TFF iliyotolewa leo na Kaimu katibu mkuu Kidao Wilfred imeeleza kuwa CAF imewajulisha TFF juu ya tuhuma hizo, zinazowahusu waamuzi wa mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Rayon Sports ya Rwanda dhidi ya Lydia Ludic Burundi Académic FC ya Burundi.

Waamuzi wa Tanzania waliochezesha mchezo huo uliomalizika kwa Rayon kushinda 1-0  huko Burundi Februari 21, ni Mfalme Ally Nassoro, Frank John Komba, Sudi Idd na Israel Mkongo Mjuni ambaye alikuwa mwamuzi wa akiba.

CAF imeieleza TFF kuwa siku koja kabla ya mchezo viongozi wa timu ya Rayon wanadaiwa kufika hotelini walipokuwa waamuzi na kuingia kwenye vyumba vyao hivyo CAF inahitaji maelezo ya waamuzi kabla ya Machi 6.

Hata hivyo TFF imeweka wazi kuwa haina nia ya kumuonea mtu bali haki itatendeka na kama watabainika kuhusika wachukuliwa hatua kali. Rayon Sports ilisonga mbele baada ya kuwa imetoka sare nyumbani ya 1-1 hivyo kuwa na ushindi wa mabao 2-1.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: