Alhamisi, 1 Machi 2018

Di maria atarajiwa kuziba pengo Neymar

ad300
Advertisement

Mchezaji Angel Di Maria amepoza machungu ya mashabiki wa Paris Saint  Germain (PSG) na kuonesha kuwa anaouwezo wa kuziba pengo la mchezaji ghali na wakimataifa Neymar Jr ambae atakua nje kwa wiki tatu.

Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu baada ya mfupa kupasuka katika mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa dhidi ya Marseille.

Mchezaji huyo ghali duniani atakosa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya matajiri wa Hispania Real Madrid unaotarajiwa kuchezwa wiki ijao mjini Paris.

Neymar ameibua hofu kwa kuwa PSG ilikuwa ikimtegemea kulipa kisasi katika mchezo baada ya kubugizwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Lakini, Di Maria ameonesha anauwezo wa kuziba pengo hilo la Neymar  baada ya juzi usiku kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu dhidi ya Marseille.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alicheza katika kiwango bora na kuiongoza Paris saint Germany ushindi wa goli tatu kwa moja. Huku akipachika mabao mawili katika mchezo huo Edson Cavan akifunga goli moja

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: