![]() |
| Advertisement |
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mheshimiwa Freemani Mbowe ameeleza kuwa Hukumu aliyopewa mheshimiwa Joseph mbilinyi sugu na katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Emmanueli Masonga ilpangwa na wao walitambua hivyo akizungumza na waandishi wa habari Mbowe ameeleza kuwa
"Hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini ni dhahiri inaoneka kuwa watawala wanaendelea kuratibu mateso kwa viongozi wa Upinzani, na tuliofahamu mapema juu ya kilichoratibiwa na tulimkataa hakini lakini bado Hakimu aliendelea kusimamia kesi hiyo na dhamira take mbaya"
Aidha Mbowe amesisitiza kuwa hawatarudi na kwamba yeye na viongozi wengine wataripoti polisi hata kama wanajua njama zilizopangwa
Nitaongoza viongozi wenzangu sita kwenda kuripoti kama Jeshi la Polisi lilivyotutaka, ingawa tunajua yanayopangwa lakini hatutaogopa na wala kurudi nyuma.
Jana jumatatu Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi Sugu na Katibu wa chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo cha miezi Mitano jera Mara baada ya kukutwa na hatia ya kuzungumza lugha ya fedhea dhidi ya rais Magufuli


0 maoni: