![]() |
| Advertisement |
Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam imetoa onyo Kali kwa wale wanaohamasisha na watakaoshiriki maandamano.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda kanda maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa amesema
Nawaomba watanzania wapenda amani wajiepushe na mpango wa watu wachache wa kuingiza nchi kwenye vurugu, ninachotaka kusema yeyote atakaeshindwa kuyapokea haya ninayosema asijutie kitakachomkuta"
Aidha Mambosasa amewaomba watanzania kudumisha hali ya amani na kujiepusha na Maandamano yanayopangwa kufanyika
"Kuna watu wanaendelea kuwahamasisha wananchi wafanye maandamano halafu wanafanya hivyo wao wakiwa wamekaa mahali salama, sasa nataka niwaambie watanzania mtu anaejua thamani ya amani ajiepushe na kwa kanda ya Dar es salaam atakaefanya maandamano asijutie yatakayotokea"
Mbali na taarifa hiyo pia kamanda wa kanda Maalumu jijini Dar es salaam ametoa taarifa ya Jeshi la polisi kumkamata
Freemasons anaefahamika kama Rajab Mohammed mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa mwenge, Rajab amekuwa akiwakamata wanawake na kuwatishia kuwanyonya damu.
Lakini pia Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kumkamata Peter Kwema maarufu kama 'BABU' anaejihusisha na ujambazi katika mikoa ya DSM, Morogoro, Arusha,Tanga na Kilimanjaro


0 maoni: