![]() |
| Advertisement |
Naibu waziri mkuu wa AUSTRALIA, BARNABY JOYCE, ambae alishinda kiti cha ubunge kwa kauli mbiu ya kujali maadili ya familia, amelazimika kujiuzulu baada ya taarifa kuvuja kuwa anakikuka maadili ya familia kwa kujihusisha kimapenzi na katibu muhtasi wake ambae anatarajiwa kujifungua mtoto wake.
Kufuatia kashfa hiyo, tayari waziri mkuu MICHELA TURNBULL,amemteua MICHAEL MACCORMACK kuchukua nafasi ya BARNABY JOYCE ambae pia amejiuzulu nafasi yake ya kiongozi wa chama chake bungeni ingawa atabakia kuwa mbunge.
Kama wanavyosema wahenga,kisa huambatana na mkasa,naibu waziri mkuu huyo sasa anakabiliwa na mashtaka mengine ya unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wanawake wengine ambao wanadai amekuwa na tabia ya kuwapapasa wanapokuwa kazini, ingawa mwenyewe amekanusha madai hayo mapya akidai kuwa hayana ukweli.


0 maoni: