Jumapili, 25 Februari 2018

Wafanyakazi 1,300 kupoteza ajira Kahama

ad300
Advertisement

Zaidi ya wafanyakazi 1,300 wamepoteza ajira zao huku Kodi ya Sh. Bilioni 28 ikikosekana baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kufungwa rasmi.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mgodi huo unaomilikiwa na Acacia, umefungwa kwa kushindwa kuzaliwa kiwango cha madini hayo kilichotarajiwa.
Kufungwa kwa mgodi huo pia kumeikosesha Wilaya ya Kahama jumla ya Sh. Bilioni 1.7 zilizokuwa zikilipwa kila mwaka, ikiwa ni mrabaha.
Uongozi wa mgodi huo umeeleza kuwa uzalishaji wa dhahabu katika eneo la mgodi umeshuka kutoka gramu 1.35 hadi 1.00 (kwa kila kilo moja ya mchanga/mawe inayochimbwa) kwa mwaka jana. Mgodi huo ulianzishwa mwaka 2009 kwa mtaji wa wawekezaji unaokaribia Sh. Trilioni moja.
Tayari mgodi huo umeanza kuuza baadhi ya mali zake yakiwamo magari, mashine, majengo na vifaa vingine. Mnada mkubwa wa kuuza mali za mgodi huo utafanyika mapema mwezi Machi, 2018

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: