Jumapili, 25 Februari 2018

Ulinzi Mkali kesi ya Sugu na Masonga

ad300
Advertisement

Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi sugu pamoja na Katibu wa chama cha chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanueli Masonga  wamewasili leo tar 26 february 2018 katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Mbeya ambapo wanashtakiwa kwa  kutumia lugha ya fedhea dhidi ya raisi John pombe Magufuli .

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya


Ulinzi umeimarishwa Katika eneo la mahakama ambapo wapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi nje ya jengo.



Hukumu inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite aliyesikiliza kesi hiyo. Upande wa mashtaka na wa utetezi ulikamilisha ushahidi Februari 9,2018.


Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.


Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.


Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa, hivyo sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.


Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.




Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: