![]() |
Advertisement |
Kada maarufu wa CCM na aliyewahi kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA), ShyRose Bhanji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa
Hakubaliani na Utawala wa Rais John pombe Magufuli na yuko tayari kwenda jela.
Mwanasiasa huyo ameeleza kuwa akaunti yake ya instargram ili kuwa hacked na hizo taarifa si za kweli
Aidha shylose ameomba msamaha kwa Raisi John pombe magufuli na wote waliokerekwa na taarifa hiyo
Ikumbukwe kuwa Mwanasiasa huyo siku kadhaa zilizopia aliandika kupitia ukurasa wake huo kuwa ''Serikali ya chama changu CCM haiwezi kukwepa lawama kwa namna yoyote ile kufuatia kupigwa risasi kwa binti ambaye hakuwa na hatia hata kidogo.
Imekuwa ni siku mbaya sana kwangu; nimeshindwa kula na nashindwa kupata usingizi kutokana na kifo cha huyu binti. Nafsi yangu inanisuta. Mungu wangu naomba unisaidie ''
0 maoni: