![]() |
| Advertisement |
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo chadema Mheshimiwa Freeman Mbowe ameeleza kuwa serikali kuwa inapotosha juu yamatukio ya Mauaji yanayoendelea nchini akizungumza na vyombo vya habari Mbowe amesema
"Mauwaji yanayotokea na yanayoendelea kutoka Serikali inapotosha kwa kusema wanaofanya mauwaji hayo hawajulikani ni dhahiri mauwaji hayo Serikali inajua wanaofanya ukali huu."
Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la hai kupitia chadema amesema kuwa wananchi wamechoshwa na matukio yanayoendelea nchini hivyo kutaka chama hicho kutoa kauli ya kulipiza kisasi juu ya matukio hayo
"Jana wakati tupo kwenye mazishi ya Godfrey J. Lweno Morogoro wananchi walikitaka Chama kitoe kauli ya kulipiza kisasi, sasa tunaanza kuona jinsi gani wanchi wameshaanza kuchoka, Chadema tunalitakia mema Taifa hili ingawa watawala hawaoni umuhimu."
Lakini pia Mbowe ameelekeza lawama kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima dhamana wahanga waliopigwa risasi akisema kuwa wanahofu wataeleza maovu ya Jeshi hilo
"Hivi sasa hivi tuna vijana waliopigwa risasi na hawajawapeleka Mahakani wala kuwapa huduma
Tunajua Jeshi la Polisi linawanyima dhamana wahanga waliopigwa risasi ili kuficha maovu ya Jeshi la Polisi wanajua wakiwaachia waandishi mtawaona na mtawahoji hii sio Tanzania tunayoijua"
Mbowe amesema kuwa hawatakata tamaa na kurudi Nyuma Mbali na Mateso ambayo upinzani unapata Mbowe amesema
"Tunamwambia Rais na wanaotekeleza mkakati huu kuwa hatutarudi nyuma, watawaumiza wengi lakini hawatakata tamaa."


0 maoni: