Jumatano, 28 Februari 2018

Lina Afunguka idadi ya wanaume aliyotembea nao

ad300
Advertisement

Msanii Linah Sanga ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake wa 'Same boy' akiwa ameshirikiana na msanii Recho amefunguka na kuweka wazi idadi ya wanaume ambao ametembea nao na kufaidi penzi lake. 




Linah Sanga akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV amesema kuwa toka amekuwa Linah na watu kumtambua kama msanii ametoka jumla ya wanaume watano japo anadai kuwa kuna wanaume wengine ambao ametoka nao kimapenzi hawakumbuki.

"Kwa haraka haraka nishatoka kimapenzi na wanaume kama watano hivi toka watu wamenifahamu kama Linah, sina idadi kubwa sana japo siwezi kuwakumbuka wote wengine nimeshawasahau kabisa, kuna watu wana idadi kubwa ya watu wametembea nao sema tu ni kwa sababu si wasaniii" alisema Linah Sanga 

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: