Jumatano, 28 Februari 2018

Dkt shein afanya mabadiliko baraza la mawaziri

ad300
Advertisement

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amafanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza Wizara moja zaidi, na kuwabadilishia Wizara baadhi ya Mawaziri.

Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za Vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo; shughli za Mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais; na shughli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Aidha, amewateua Naibu Mawaziri wapya wawili na kumbadilisha Wizara Naibu Waziri mmoja. Kufuatia mabadiliko hayo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivi sasa itakuwa na Wizara 14 zenye Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi- Mheshimiwa Issa Haji Ussi Gavu

3. OFISI YA RAIS, KATIBA SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NAUTAWALA BORA

4. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman

5. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora – Mheshimiwa Khamis Juma Mwalim

6. OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

7. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Haji Omar Kheri

8. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ – Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis

9. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
10. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed

11. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – Mheshimiwa Mihayo Juma Nhunga

12. WIZARA YA AFYA

13. Waziri wa Afya- Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed

14. Naibu Waziri wa Afya – Mheshimiwa Harusi Said Suleiman

15. WIZARA YA ARDHI, NYUMBA, MAJI NA NISHATI

16. Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Salama Aboud Talib

17. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati – Mheshimiwa Juma Makungu Juma

18. WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA

19. Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Balozi Amina Salim Ali

20. Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda – Mheshimiwa Hassan Khamis Hafidh

21. WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

22. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma

23. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amal Mheshimiwa Mmanga Mjengo Mjawiri

24. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

25. Waziri wa Fedha na Mipango – Mheshimiwa Dkt. Khalid Salum Mohamed

26. WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE

27. Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo

28. Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Choum Kombo Khamis

29. WIZARA YA KAZI, UWEZESHAJI, WAZEE, WANAWAKE NA WATOTO

30. Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mheshimiwa Maudline Cyrus Castico

31. Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto –
Mheshimiwa Shadia Mohamed Suleiman

32. WIZARA YA KILIMO, MALIASILI, MIFUGO NA UVUVI

33. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Rashid Ali Juma

34. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi – Mheshimiwa Dkt. Makame Ali Ussi

35. WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI

36. Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Dkt. Sira Ubwa Mamboya

37. Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji – Mheshimiwa Mohamed Ahmada Salum

38. WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

39. Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Balozi Ali Abeid Karume

40. Naibu Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo – Mheshimiwa Lulu Msham Abdulla

Aidha, Mheshimiwa Said Soud Said na Mheshimiwa Juma Ali Khatib
wanaendelea kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum.

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: