![]() |
Advertisement |
USISAHAU: Maswali muhimu kutoka Ripoti ya CAG 2016/17 SERIKALI KUU
( rejea kurasa za Ripoti Kuu ya CAG )
- Zipo wapi TZS 1.5trn zilizokusanywa na Serikali Lakini hazikutolewa kwa matumizi wala kukaguliwa? Ukurasa 34
- Kwanini Serikali imekopa TZS 500bn zaidi ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge. Uk 30
- Kwanini Serikali imetekeleza 68% tu ya Bajeti ya Maendeleo kwa Serikali Kuu na 51% tu kwa Serikali za Mitaa? uk 38
- Kwanini Serikali ilitumia zaidi ya shilingi 219 bilioni, kulipa madeni ya nyuma ambayo hayakuwa kwenye Bajeti? uk 40
- Kwa nini TRA Wametoa Takwimu za Uongo za Mapato ya Kodi ya zaidi ya shilingi 2.2 trilioni? uk 109
- Serikali ya Jamhuri ya Muungano imepata Hati Chafu ( Hesabu Jumuifu za Taifa ). Kwanini Katibu Mkuu Hazina hajachukuliwa hatua kama ilivyokuwa kwa Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa? uk 296-298
0 maoni: