Ijumaa, 13 Aprili 2018

Seneta aliyepinga matumizi ya kiswahili katika mtandao wa facebook ashutumiwa

ad300
Advertisement

Kauli ya dharau ya Seneta wa Republican, John Kennedy ya kumtaka Ofisa Mtendaji mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg asitumie Kiswahili bali Kiingereza ambacho kila raia wa Marekani anaweza kuielewa imeshutumiwa na maseneta wenzake.
Seneta huyo alishutumiwa wakati wa kikao cha kamati mbili – Kamati ya Bunge ya Sheria na Kamati ya Bunge ya Biashara – zilipokuwa zinasikiliza utetezi wa kiongozi huyo wa mtandao wa jamii juu ya shutuma zilizoelekezwa kwake kuhusu ukiukwaji wa sera ya faragha na udhibiti.

"Ninapendekeza kwamba urudi nyumbani ukaandike upya na uwaambie wanasheria wako unaowalipa dola za Marekani 1,200 kwa sasa, sikukosei heshima, ni wazuri, lakini waambie kwamba unataka iandikwe kwa Kiingereza na si Kiswahili, ili Mmarekani wa kawaida aweze kuelewa. Huo utakuwa mwanzo,” alisema.

Kadhalika Kennedy alilalamika kwamba makubaliano ya mtumiaji wa Facebook yalifanywa kuwa magumu sana na yalianzishwa ili kulinda mtandao huo wa kijamii usishtakiwe badala yake uwe njia ya kuwafanya watumiaji kujua haki zao.
Lakini Kennedy alishutumiwa kwa namna alivyotumia neno "siyo Kiswahili" wengi wakidai kuwa ni mbaguzi.

Licha ya maneno hayo ya hasira, Seneta Kennedy alikataa kuomba msamaha kwa kauli hiyo. Wakati wa mahojiano na mtangazaji wa CNN Erin Burnett, Kennedy alisema: "Hakukuwa na jambo la kuomba radhi. Nafikiri kila mmoja alielewa hoja ambayo nilijaribu kusisitiza."

Share This
Previous Post
Next Post

Pellentesque vitae lectus in mauris sollicitudin ornare sit amet eget ligula. Donec pharetra, arcu eu consectetur semper, est nulla sodales risus, vel efficitur orci justo quis tellus. Phasellus sit amet est pharetra

0 maoni: