![]() |
Advertisement |
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt John pombe magufuli amezindua ukuta uliojengwa kuzunguka mgodi wa Tanzanite uliopo mkoani Manyara ukuta huo uliagizwa kujengwa na mheshimiwa raisi kutokana na upotevu wa madini na wizi katika mgodi huo akizungumza katika uzinduzi huo
Mkuu wa jeshi la kujenga taifa (JKT) Martini Busungu ametoa taarifa ya ujenzi wa ukuta huo, na amemshukuru Mkuu wa majeshi ya Ulinzi,Salvatory Mabeyo kwa kuanza kutoa maagizo juu ya ujenzi wa ukuta huo baada ya rais kusema ujengwe
Amewashukuru pia Tanroads, na taasisi ya wahandisi Tanzania, kiwanda cha Saruji Tanga kwa kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mradi huo
Anasema ujenzi wa ukuta huo umejengwa kwa utaalamu wa kutosha kwakutumia wataalamu wake wa jeshi
Gharama za ujenzi wa maradi huo ni Shilingi 5,645,843,163, maradi huo ulikabiliwa na changamoto kama ujenzi kwenye miamba na makorongo na uwepo wa mito ya misimu
Ujenzi huoulifanyika kwa njia ya operesheni ambapo vijana wa JKT walitumika katika ujenzi na kutoa maelekezo ya kitaalamu
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mabeyo
Amesema kuwa taifa hili limeweka historia itakayodumu milele, ukuta huo uliagizwa kujengwa mwezi Septemba mwaka 2017.
Maagizo hayo yametekelezwa na kazi imekamilika na watamkabidhi ndani ya muda mfupi ujao, ukuta huo una urefu wa kilomita 24.5 na ulianza kujengwa mwezi Novemba mwaka 2017 na kukamilika mwezi Februari mwaka 2018
Waliokamilisha ujenzi huo ni waandisi kutoka JKT pamoja na askari wa JKT
Fedha zilizotumika kujenga zinaoweza kuonekana ni nyingi, ila gharama hizo zitaonekana ni ndogo ukuta huo utakapoanza kuleta manufaa
Taifa linapaswa kujivunia kutokana na ujenzi wa ukuta huo, ujenzi wa ukuta huo unaonyesha kuwa jukumu la jeshi sio kulinda mipaka ya nchi na katiba ya nchi tu, bali pia kushiriki katika ujenzi wa miradi inayosaidia kujenga taifa
Katika utekelezaji wa jukumu hilo kumejidhihirisha, uzalendo, umoja na mshikamano katika watanzania wapenda maendeleo, kwani walipata msaada kutoka katika wananchi wa eneo la Mererani
Pia JKT wametumia uweo wao kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu
Jeshi limeonyesha nidhamu ya juu katika uchapaji kazi katika utekelezaji wa maagizo yanayotolewa, mradi huo ulipangwa kukamilika ndani ya miezi 6 ila ulkikamilika katika miezi 3
Maagizo pia ya ujenzi wa ukuta katika uwanja vita wa Ngerengere nao unajengwa na upo katika hatua za mwisho, ukuta huo una urefu wa kilometa 14 na wanaoshiriki katika ujenzi huo ni vijana waiojenga ukuta wa Mererani
Mkuu wa majeshi anahitimisha kwa kusema muda wowote wapo tayari kutekeleza maagizo yoyote yatakayoagizwa kwa ajili ya maslahi ya nchi
Lakini pia Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi amemshukuru rais kwa imani aliyonayo kwa jeshi tanzania na wizara yake, na pia kukubali kuhudhuria uzinduzi wa ukuta huo licha ya kua na majukumu mengi
Anasema ukuta huo utakuwa historia katika nchi yetu kwani eneo lenye rasilimali muhimu ya nchi linalindwa kwa kujengewa ukuta
Pia ameshukuru jeshi la Tanzania kwa utekelezaji wa ujenzi huo kwa weledi na ndani ya muda mfupi
Pia ameshukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano kwa jeshi wakati wa ujenzi wa ukuta huo hadi ukakamilika
Kwa upande wake raisi dkt John pombe magufuli Amempongeza Jenerali Mabeyo kuwa hicho ndio kilikuwa kipimo chake na amekishinda, maana hakuna aliyetegema ukuta huo kuchukua muda mrefu
Raisi amesema wangeweka kandarasi ukuta huo ungechukua zaidi ya mwaka na vifaa vya ujenzi vingeibiwa
Rais anasema maombi yaliyoombwa hapo kuhuhusu kuwafukiria vijana waliojenga ukuta huo ni ngumu kuyakataa
Anashukuru wizara ya madini na ulinzi na majemedari wote hadi wa chini kwa jinsi walivyosimamia ujenzi wa ukuta huo
Anaahidi waziri wa ujenzi na CDF kuwa atatoa barua yake yakuwashukuru walioshiriki ujenzi wa ukuta huo na ataangalia utaratibu mzuri wa kuwapongeza
0 maoni: